Pata taarifa kuu
ZIMBABWE- SIASA

Wanasiasa wa upinzani 25 wanazuiliwa na polisi Zimbabwe

Wanasiasa wa upinzani 25 wakiwemo wafuasi wao, wanashikiliwa na jeshi la polisi nchini Zimbabwe, baada ya kuvamiwa wakati wakiendelea na mkutano, tukio linalojiri miezi michache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa rais na wabunge.

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari.
Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Nelson Chamisa katika mkutano na waandishi wa habari. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa waliokamatwa ni kutoka muungano wa kisiasa wa Citizens Coalition for Change, unaoongozwa na kinara wa upinzani Nelson Chamisa.

Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanazungumziaje tukio hili na kinachoendelea nchini Zimbabwe, Hamduni Marcel, anaangazia hili akiwa Mwanza, Tanzania.

Kukamatwa kwa wapinzani nchini Zimbabwe ni ishara kuwa bado hali  si shwari.amesema Hamduni Marcel.

Baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani katika mataifa barani Afrika yamekuwa yakizituhumu serikali zilizoko madarakani kwa ukandamizaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.