Pata taarifa kuu
DHULMA-HAKI

Mwendesha mashtaka wa ICC ataka kumfungulia mashtaka Joseph Kony

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) amesema Alhamisi aliomba majaji kuthibitisha mashtaka dhidi ya mwanzilishi wa kundi la waasi nchini Uganda la Lord's Resistance Army (LRA) Joseph Kony, ambaye yuko mafichoni kwa zaidi ya miaka 17.

Joseph Kony. Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) amesema Alhamisi amewataka majaji kuthibitisha mashtaka dhidi ya mwanzilishi wa kundi katili la waasi wa Uganda la LRA.
Joseph Kony. Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) amesema Alhamisi amewataka majaji kuthibitisha mashtaka dhidi ya mwanzilishi wa kundi katili la waasi wa Uganda la LRA. Reuters/Stuart Price/Pool
Matangazo ya kibiashara

"Bw. Kony amejaribu kukwepa haki kutoka kwa Mahakama hii kwa zaidi ya miaka 17," mwendesha mashtaka wa ICC Karim Khan amesema katika taarifa yake, na kuongeza kuwa ni mara ya kwanza ofisi yake kuomba kikao cha majaji cha uthibitisho wa kusikilizwa kwa mashtaka bila kuwepo mtuhumiwa.

Hati ilitolewa mwaka wa 2005 kwa Joseph Kony, mwanzilishi na kiongozi wa Lord's Resistance Army, anayeshtakiwa kwa makosa 33 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, ukatili, utumwa, ubakaji na mashambulizi dhidi ya raia.

"Ninaamini sasa inafaa na ni muhimu kuendeleza kesi dhidi yake kwa kiwango kinachoruhusiwa na masharti ya Mkataba wa Roma", ulioanzisha ICC, amesema Bw. Khan.

"Sambamba na hilo, afisi yangu itaimarisha juhudi zake za kufanikisha kukamatwa kwa Bw. Kony, ambaye pia anasalia kuwa mshukiwa aliyemafichoni anayetafutwa kwa muda mrefu na ICC," ameongeza. "Kuthibitishwa kwa mashtaka bila kuwepo Bw. Kony na kukamatwa kwake kutafungua njia ya kupangwa kwa kesi yake haraka iwezekanavyo", amesisitiza.

Kundi la waasi la LRA ambalo lilianzishwa nchini Uganda katika miaka ya 1980 na mvulana wa zamani wa madhabahu Joseph Kony ili kuanzisha utawala unaozingatia Amri Kumi za Mungu, lilihatarisha maeneo makubwa ya Afrika ya Kati kwa miaka 30 kwa kuwateka nyara watoto, kuwakata raia viungo vyao na kuwafanya wanawake kuwa watumwa.

Anahusika na vifo vya zaidi ya watu 100,000 na utekaji nyara wa watoto 60,000, wavulana waliogeuzwa kuwa wanajeshi na wasichana wadogo kuwa watumwa wa ngono.

Kundi hili la LRA ambalo lilifukuzwa nchini Uganda, limetawanyika katika misitu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini na Sudan.

ICC haiwezi kumshtaki mshukiwa asipokuwepo lakini inaweza kushikilia uthibitisho wa kusikilizwa kwa mashtaka bila kuwepo kwake, kulingana na Khan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.