Pata taarifa kuu

Ujerumani kuondoa wanajeshi wake nchini Mali ifikapo mwishoni mwa mwaka 2023

Ujerumani inakusudia kuondoa wanajeshi wake kutoka Mali ifikapo "mwishoni mwa mwaka 2023", na hivyo kumaliza ahadi yake ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika nchi hii (MINUSMA), chanzo cha serikali kimeliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano.

Mwanajeshi wa Ujerumani kutoka MINUSMA, Gao, Mali, Agosti 2018.
Mwanajeshi wa Ujerumani kutoka MINUSMA, Gao, Mali, Agosti 2018. AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

"Wanajeshi wa Ujerumani watasitisha ushiriki wao katika operesheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa MINUSMA ifikapo mwishoni mwa mwaka 2023," chanzo kimesema kwa sharti la kutotajwa jina.

Uamuzi huu ni makubaliano ya kimsingi ndani ya serikali ya Ujerumani na tangazo rasmi litatolewa Jumanne ya wiki ijayo, kulingana na chanzo hicho.

Nchi kadhaa zimejitolea kutathmini upya ushiriki wao katika MINUSMA kutokana na kuongezeka kwa ukosefu wa usalama. Nchi za magharibi zinashutumu hasa uwepo wa mamluki wa kundi la Wagner kutoka Urusi, waliokuja Mali kwa wito wa utawala wa kijeshi unaoongoza nchi hiyo.

Takriban wanajeshi 1,100 wa Bundeswehr wanashiriki katika kikosi cha MINUSMA, kilichozinduliwa mwaka 2013 na chenye lengo la kuimarisha usalama katika nchi hii ya Afrika Magharibi inayokumbwa na mashambulizi ya wanajihadi.

Mamlaka ya wanajeshi wa Ujerumani nchini Mali inaendelea hadi mwishoni mwa mwezi wa Mei 2023.

Mji wa Gao, ulioko mashariki mwa Mali, ni makazi ya kambi kuu ya jeshi la Ujerumani. Vikosi vya Ujerumani vinashiriki hasa katika ulinzi wa uwanja wa ndege. 

Serikali ya Ujerumani ilitangaza katikati ya mwezi wa Agosti kwamba ilikuwa na habari kwamba Warusi walikuwapo kwenye uwanja wa ndege wa Gao. Uingereza na Côte d'Ivoire zilitangaza wiki hii kuondoa vikosi vyao nchini Mali.

Ufaransa, iliyoingilia kijeshi nchini Mali, hasa kupitia wanajeshi wa kikosi cha Barkhane, iliamua mnamo Februari kuondoa wanajeshi wake. Wanajeshi wa mwisho wa Ufaransa waliondoka Mali msimu huu wa joto, baada ya karibu muongo mmoja wakihudumlu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.