Pata taarifa kuu

Malawi: Kambi za wakimbizi zajaa kupita kiasi kufuatia wimbi la wakimbizi kutoka DRC

Nchini Malawi, idadi ya wakimbizi wa Kongo inaendelea kuongezeka. Wanakimbia mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kutokana na hali hii, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, linatoa tahadhari. Kambi pekee ya wakimbizi nchini ina uwezo wakupokea watu 10,000, lakini wakimbizi waliko katika kambi hiyo ni mara tano zaidi ya idadi.

Kambi ya wakimbizi ya Dzaleka nchini Malawi mwaka 2018. Wakimbizi wengi wa Kongo wamekuwa wakiwasili Malawi tangu kuzuka upya kwa mapigano mashariki wa DRC.
Kambi ya wakimbizi ya Dzaleka nchini Malawi mwaka 2018. Wakimbizi wengi wa Kongo wamekuwa wakiwasili Malawi tangu kuzuka upya kwa mapigano mashariki wa DRC. © AMOS GUMULIRA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Takriban kilomita arobaini kutoka Lilongwe, mji mkuu wa Malawi, kambi ya Dzaleka ni makazi ya wakimbizi 56,000, asilimia 62 kati yao wakiwa nia raia wa DRC. Wanaishi pamoja na Warundi, Wanyarwanda, Waethiopia na Wasomali. Katika miezi ya hivi karibuni, mapigano yalizuka tena mashariki mwa DRC kati ya waasi wa kundi la M23 na wanajeshi wa DRC, FARDC. Kurejea kwa kundi hili lililoshindwa mwaka 2013 kulileta wimbi jingine la wakimbizi na kusababisha idadi kubwa ya wakimbizi katika kambi iliyojaa ya Dzaleka.

Hali ya kibinadamu ambayo imekuwa ngumu kwa mujibu wa Mpango wa Chakula Duniani. Hivi majuzi, familia 600, kati ya 11,000 katika kambi hiyo, zililazimika kuondolewa kwenye orodha ya wanufaika wa mgao wa chakula, kwa kukosa njia. Na kwa mujibu wa mwakilishi wa jumuiya ya Wakongo katika kambi ya Dzaleka, baadhi ya wakimbizi "wanalala njaa" na hatari ya kufa njaa.

Kwa mujibu wa WFP, uhaba wa chakula ni moja ya athari kubwa ya kutoroka kwa raia nchii Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tangu mapigano yalipozidi Oktoba 20, 2022, Wakongo wasiopungua 183,000 wameyakimbia makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.