Pata taarifa kuu

Maelfu waandamana dhidi ya Rwanda mjini Goma

Maelfu kadhaa ya watu wenye hasira wameandamana Jumatatu mjini Goma dhidi ya Rwanda, wakishutumiwa na mamlaka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao wamejiimarisha katika siku za hivi karibuni mashariki mwa nchi hiyo, wanahabari wa shirika la habari la AFP wameshuhudia.

Maaandamano yalifanyika katika eneo hili liitwalo kituo cha mpaka cha Grande Barrière huko Goma.
Maaandamano yalifanyika katika eneo hili liitwalo kituo cha mpaka cha Grande Barrière huko Goma. © Paulina Zidi / RFI
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji hao, wakiwemo mamia ya waendesha baiskeli, wengine wakiwa na fimbo na mawe, waliingia katika mitaa ya mji huo wenye wakazi zaidi ya milioni moja, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini. Kisha walielekea kwenye "kizuizi kikubwa", kituo cha mpakani kati ya DRC na Rwanda, kabla ya kutawanywa na polisi wa Kongo kwa mabomu ya machozi.

"FARDC (jeshi la DRC), tupeni silaha", waliimba waandamanaji hawa, pamoja na kauli mbiu za chuki dhidi ya Rwanda na Uganda. “Tumechoka, leo tutaingia Rwanda!” Mwandamanaji mmoja amesema.

"Tunalaani unafiki wa jumuiya ya kimataifa mbele ya uvamizi wa Rwanda. Tunateseka kwa sababu ya Rwanda, inatosha. Tunataka kutuma ujumbe kwa (Rais wa Rwanda Paul Kagame)", Mambo Kawaya, mwakilishi wa shirika la kiraia ametangaza katikati ya umati wa watu.

Tayari siku ya Jumapili, makumi ya vijana waliandamana na kuchoma bendera ya Rwanda huko Goma.

Kundi la M23 ("Movement of March 23") ni waasi wa zamani wengi wao kutoka jamii ya Watutsi ambao walichukua silaha tena mwishoni mwa 2021, wakiishutumu Kinshasa kwamba haikuheshimu makubaliano ya kuwarejeshawapiganaji wa kundi hilo katika maisha ya kiraia na wengine kuingizwa katika jeshit. DRC inaishutumu Rwanda kwa kuunga mkono uasi huu, ambao Kigali inakanusha.

Baada ya miezi kadhaa ya mvutano kati ya majirani hao wawili, Kinshasa iliamua Jumamosi kumfukuza balozi wa Rwanda nchini DRC, baada ya waasi wa M23 kuteka miji ya Kiwanja na Rutshuru-centre, iliyoko kwenye barabara ya kitaifa 2, baraara la kimkakati linalotumiwa kwa kuingiza chakula katika mji huo. Mwezi Juni, kundi hilo la waasi liliteka mji wa Bunagana, kwenye mpaka wa Uganda.

Mnamo miezi ya Novemba na Desemba 2012, waasi wa M23 waliikalia Goma kwa siku kumi, kabla ya kushindwa mwaka uliofuata na vikosi vya jeshi vya Kongo na walinda amani wa Umoja wa Mataifa, baada ya miezi 18 ya vita vya msituni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.