Pata taarifa kuu
MAADHIMISHO-HAKI

Senegal: Miaka 20 baada ya kuzama kwa feri 'Joola', matarajio bado ni mengi kwa waathiriwa

Nchini Senegal  leo ni kumbukumbu ya miaka 20 tangu kutokea kwa ajali ya Ferry, MV Le Joola , Pwani ya Gambia na kusababisha vifo vya karibu watu 2,000.  Familia za watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo wanaomba fidia lakini pia kujengewa mnara, wa kuwakumbuka wapendwa wao. 

Mnamo Septemba 26, 2002, Joola, feri iliyosafiri kati ya Dakar na Ziguinchor, ilizama kwenye pwani ya Gambia. Serikali inasema watu 1,863 walikufa maji, huku mashirika ya waathiriwa yakidai zaidi ya vifo 2,000.
Mnamo Septemba 26, 2002, Joola, feri iliyosafiri kati ya Dakar na Ziguinchor, ilizama kwenye pwani ya Gambia. Serikali inasema watu 1,863 walikufa maji, huku mashirika ya waathiriwa yakidai zaidi ya vifo 2,000. AFP PHOTO
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Septemba 26, 2002, Joola, feri iliyosafiri kati ya Dakar na Ziguinchor, ilizama kwenye pwani ya Gambia. Serikali inasema watu 1,863 walikufa maji, huku mashirika ya waathiriwa yakidai zaidi ya vifo 2,000.

Maadhimisho yalianza Jumatatu hii saa 10:30 kwa kuweka shada la maua na maombi katika makaburi ya Kantène. Sherehe rasmi inafanyika katika bandari ya Ziguinchor wakiwepo viongozi mbalimbali wa nchi hiyo, familia na ndugu wa waathriwa, pamoja na walionusurika. Miaka 20 iliyopita, abiria 64 pekee ndio walionusurika katika ajali hiyo ya feri 'Joola' katika pwani ya Gambia.

Léandre Coly ni mmoja wao. Alikuwa na umri wa miaka 37 mnamo Septemba 26, 2002. Miaka 20 baadaye, muumini huyu wa kanisa Katoliki anasema hana kinyongo na mtu yeyote. “Nina moyo wa huruma. Ninashukuru kuwa hapa kuzungumza. Lakini hiyo haimaanishi kwamba ninasahau watu waliofariki katika ajali hiyo mbaya. Linapaswa kuwa somo, ” amesema.

"Roho ziko chini ya bahari na huzungumza nasi kila siku. Wanatunyoshea mkono ili tuje kuwachukua. Uvimbe unawapiga, unawaua, kwa sababu bahari sio makaburi. Tunapaswa kuwatoa. Hii ingetuwezesha kujiweka huru, kuomboleza. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.