Pata taarifa kuu

EU kutoa msaada wa Dola Milioni 15 kusaidia jeshi la SAMIM Msumbiji

Umoja wa Ulaya umetangaza kutoa msaada wa Dola Milioni 15 kusaidia jeshi kutoka mataifa ya Afrika chini ya Jumuiya ya Kiuchumi ya SADC SAMIM, linalokabiliana na wanajihadi.

Msafara wa wanajeshi wa Afrika Kusini wakiwa katika barabara ya Maringanha kuelekea Pemba. Afrika Kusini ina kikosi kikubwa zaidi cha SADC kilichopo Msumbiji. Agosti 5, 2021.
Msafara wa wanajeshi wa Afrika Kusini wakiwa katika barabara ya Maringanha kuelekea Pemba. Afrika Kusini ina kikosi kikubwa zaidi cha SADC kilichopo Msumbiji. Agosti 5, 2021. AFP - ALFREDO ZUNIGA
Matangazo ya kibiashara

Msaada huo unatarajiwa kusaidia kujenga amani nchini Msumbiji, lakini pia kuimarisha jeshi la polisi, kuwezesha mazungumzo na mashirika ya kiraia kwa lengo la kuimarisha uongozi bora na utii wa sheria. 

Pamoja na hayo, msaada huu unalenga kulisaidia jeshi hilo kutoka mataifaya SADC kupata magari, boti na vifaa vya tiba, kwa lengo la kuwasaidia katika operesheni zao. 

Umoja wa Ulaya unasema, kupitia kwa msaada huu, unalenga kuisaidia Msumbiji kupata utulivu na usalama, hasa Kaskazini mwa nchi hiyo, tangazo linalokuja wakati huu mkuu wa sera wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell, akizuru Msumbiji. 

Tangu mwaka 2017, mkoa wenye utajiri wa Cabo Delgado ulianza kushuhudia utovu wa usalama baada ya kuzuka kwa wanajihadi ambao wametatiza usalama wa raia katika eneo hilo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.