Pata taarifa kuu

IMF yaidhinisha mkopo wa dola milioni 456 kwa Msumbiji.

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limetia saini mkopo wa dola milioni 456 kwa ajili ya serikali ya Msumbiji, ikiwa ni msaada wa kwanza wa aina hiyo kutolewa tangu kashfa ya deni kuzuka miaka sita iliyopita nchini humo.

IMF-ASIA
IMF-ASIA REUTERS - Johannes Christo
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya kukamilisha makubaliano hayo inaashiria kurejea kwa mara nyingine tena kwa Msumbiji katika hali nzuri baada ya kutokea kwa kashfa ya deni, wakati serikali ilipochukua mikopo ya dola bilioni 2 ambayo haikutoa taarifa bungeni, kwa umma wala kwa wakopeshaji wengine.

IMF imesema katika taarifa yake kwamba Mpangilio wa miaka mitatu utasaidia kufufua uchumi na sera za kupunguza deni la umma na udhaifu wa kifedha, mpango unaunga mkono ajenda kabambe ya mageuzi ya mamlaka.

Kashfa hiyo ilisababisha mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi wa Msumbiji tangu pale ilipo pata uhuru kutoka kwa Ureno miongo minne iliyopita.

Serikali ilipata mikopo ya siri ya dola bilioni 2 sawa na (euro bilioni 1.8) mwaka wa 2013 na 2014 kutoka kwa benki za kimataifa ili kununua meli za uvuvi na meli za uchunguzi.

Mkopo huu unatarajiwa kuisaidia Msumbiji sio tu katika maswala ya kiuchumi bali pia utapiga jeki vita dhidi ya makundi ya kijihadi yanyaoendeleza shughuli zake katika eneo la Cabo delgado eneo lenye utajiri wa gesi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.