Pata taarifa kuu
USALAMA-HAKI

Ethiopia: UNICEF yalaani shambulizi la anga dhidi ya shule la 'chekechea' Mekele

Nchini Ethiopia, shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto,  UNICEF, linalaani shambulizi la anga lililofanywa Ijumaa Agosti 26) katika mji mkuu wa  Tigray, Mekeledhidi ya 'shule ya chekechea'.

Hapa ni sokoni katika jimbo la Ethiopia la Tigray, Mei 2021.
Hapa ni sokoni katika jimbo la Ethiopia la Tigray, Mei 2021. © RFI/ Sébastien Németh
Matangazo ya kibiashara

Mapigano yalianza tena Jumatano, Agosti 24, kaskazini mwa Ethiopia kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Tigraya, na hivyo kusitisha makubaliano ya miezi mitano. 

Siku ya Ijumaa Agosti 26, shambulio la anga lililotekelezwa na vikosi vya Ethiopia kwenye mji wa Mekele, mji mkuu wa Tigray, liliripotiwa kuwaua watu wanne, wakiwemo watoto wawili.

"Kwa mara nyingine, watoto wamelengwa kutokana na kuongezeka kwa uhasama," limeshutumu shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, UNICEF , katika taarifa kwa vyombo vya habari. Kwa takriban miaka miwili, watoto na familia zao katika eneo hilo wamekumbwa na hali ya kutisha ya mzozo huu. Ni "lazima ikome", limeongeza shirika hilo.

"Mabomu kwenye eneo la makazi"

Lawama hii ya UNICEF ​​​​ni uthibitisho wa kwanza wa kimataifa kwamba shule ya chekechea imesambuliwa, kama ilivyodaiwa na mamlaka ya waasi huko Tigray. Kulingana na waasi hao, ndege ya kijeshi "ilidondosha mabomu kwenye eneo la makazi na shule ya chekechea huko Mekele" asubuhi ya Ijumaa tarehe 26 Agosti.

Serikali ya Ethiopia inakanusha shutuma hizi, ikiongeza kuwa vikosi vya anga vya Ethiopia vinalenga tu "maeneo ya kijeshi" na inawashutumu waasi kwa kupotosha ukweli wa mambo. Mkurugenzi wa Hospitali ya Mekele, aliyehojiwa na shirika la habari la AFP, anabaini kwamba kituo chake kilipokea, siku ya Ijumaa, watu wanne waliofariki wakiwemo watoto wawili na tisa waliojeruhiwa.

Mapigano yalianza tena Jumatano Agosti 24 kati ya serikali ya shirikisho na mamlaka ya waasi huko Tigray. Pande hizo zinashtumiana kwa kila upande kuhusika kwa kuanzisha tena uhasama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.