Pata taarifa kuu
Nigeria - usalama

Nigeria : Polisi wauawa na watu wenye Silaha

Mamlaka nchini Nigeria zimesema watu wenye silaha wamewaua watu 17, wakiwemo polisi watano kwenye mambulizi mawili tofauti, katika jimbo la Katsina.

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari.
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari. AP - Julien de Rosa
Matangazo ya kibiashara

Watu hao wenye silaha wanasemekana kuvamia kituo cha polisi cha Kankara, na kuwamiminia risasi polisi watano waliofariki papo hapo, kisha baadaye wakawaua raia watatu .

Katika kisa kingine tofauti watu wenye silaha walivamia vijiji kadhaa katika wilaya ya Faskari, na kuwaua watu 9, kabla ya kutoweka na mifugo na vyakula.

Jimbo la Katsina, nyumbani kwa rais Muhammadu Buhari, ni moja kati ya majimbo nchini Nigeria yanayoendelea kushuhudia utovu wa usalama, wakati huu serikali ikiendelea kukosolewa kwa kushindwa kupambana na wanajihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.