Pata taarifa kuu
Nigeria - Elimu

Nigeria : Rais Buhari aagiza mawaziri kumaliza mgomo wa wahadhiri

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ,ameagiza mawaziri wa elimu na kazi nchini humo kumaliza mgomo wa muda mrefu wa wahadhiri.

Rais wa Nigeria, Buhari
Rais wa Nigeria, Buhari © Nigeria presidency
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa wahadhiri nchini Nigeria, (ASUU), umeongoza mgomo huo tangu mwezi Februari tarehe 14 mwezi huu.

Wahadhiri hao wanagoma kushinikiza serikali kutekeleza mkataba wao wa mwaka 2009, uliolenga kuhakikisha wanapata nyongeza ya mishara mbali na miundo mbinu ya vyuo vikuu kuimarishwa, wahadhiri hao wanasisitiza mgomo huo utawafaidi zaidi wanafunzi, licha ya kuchukuwa muda wao.

Juhudi za serikali na viongozi wa wahadhiri kushiriki mazungumzo kumaliza mgomo huo hazijafua dafu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.