Pata taarifa kuu
Togo - usalama

Togo : Jeshi lakiri kuwaua vijana saba na kuomba msamaha

Jeshi nchini Togo limeomba msamaha kwa kuwaua vijana saba ambao linasema lilifikiri ni wanajihadi.

Wanajeshi wa Togo
Wanajeshi wa Togo AFP - PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Kupitia taarifa mkuu wa jeshi nchini humo jenerali Dadja Maganawe, amesema wanajishi walitekeleza mauwaji hayo baada ya ndege ya kivita iliokuwa inafanya doria kushambuliwa usiku.

Vijana waliouawa ni kati ya umri wa miaka 14 hadi 18, ambao vyombo vya habari  eneo la Savanes, nchini Togo, vimesema walikuwa wanarejea nyumbani baada ya kuhudhuria sherehe za Eid al Adha.

Jeshi nchini Togo limekuwa likishika doria usiku na mchana katika miji mbalimbali baada ya shumbulio la kwanza dhidi yao lililotekelzwa na wanajihadi karibu na mpaka wa Burkina faso na kusabisha vifo vya wanajeshi 8.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.