Pata taarifa kuu

Wanajeshi wanane wa Togo wameauwa baada ya kushambuliwa na magadi.

Wanajeshi wanane wa Togo wameauwa na wengine 13 kujeruhiwa baada ya kushambuliwa na magaidi Kaskazini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Burkina Faso. 

 Rais wa Togo Faure Gnassingbé.
Rais wa Togo Faure Gnassingbé. PIUS UTOMI EKPEI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Togo imethibitisha kutokea kwa mauaji dhidi ya vikosi vyake, vinavyopambana na wanajihadi Kaskazini mwa nchi yake. 

Mpaka sasa hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika na shambulio hilo ambalo linaelezwa, lilitekelezwa na kundi la watu zaidi ya sitini waliokuwa na silaha, wakiwa kwenye pikipiki. 

Makabiliano hayo yanaelezwa yalidumu kwa zaidi ya saa mbili, kabla ya Togo kutuma vikosi zaidi. 

Mwezi Novemba mwaka uliopita, wanajeshi wa Togo walizuia shambulio la kigaidi Kaskazini mwa nchi hiyo kabla ya shambulio la Jumatano. 

Wiki iliyopita, kulikuwa na mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi katika nchi za Afrika Magharibi Magharibi walikutana kujadili hali ya usalama katika êneo hilo ambalo limeendelea kukabiliwa na utovu wa usalama, na ikabainika kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na matukio zaidia ya Elfu tano ya kigaidi na kusababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 16. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.