Pata taarifa kuu
Chad - Siasa

Chad : Serikali yatangaza kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa

Serikali ya kijeshi ya mpito nchini Chad, imesema mazungumzo ya kitaifa kuelekea kuandaliwa kwa uchaguzi wa mwaka ujao, yataanza Agosti 20.

Mahamat Idriss Déby, rais wa Baraza la Kijeshi la Mpito nchini Chad, na mtoto wa marehemu Rais Idriss Déby Itno kwenye mazishi ya baba yake, Aprili 23, 2021
Mahamat Idriss Déby, rais wa Baraza la Kijeshi la Mpito nchini Chad, na mtoto wa marehemu Rais Idriss Déby Itno kwenye mazishi ya baba yake, Aprili 23, 2021 AFP - CHRISTOPHE PETIT TESSON
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya kitaifa ni ahadi iliotolewa na rais wa mpito, Mahamat Idriss Déby, baada ya kuingia madarakani kufutia kifo cha babake mwaka uliopita.

Wanahakatai na jamii ya kitaifa wamekuwa wakishinikiza utawala wa kijeshi nchini Chad, kurejesha serikali ya kiraia.

Mwachama wa kamati ya bunge la seneti nchini Marekani, Bob Menendez, amesema Marekani itamuekea vikwazo rais Deby na jeshi, iwapo mchakato wa kurejesha utawala wa kiraia hautafaulu.

Vuguvugu la maandamano la Wakit Tamma, tayari limeitisha maandamano hapo kesho kutaka  utawala wa kijeshi kuwahakikishia raia kwamba wanajeshi hawatashiriki uchaguzi wa mwaka ujao.

Wakit Tamma pia linataka majibu kutoka kwa serikali kuhusu muda wa serikali ya mpito na ni lini wanajeshi wa Ufaransa wataondoka nchini Chad, Wakit Tamma likituhumu Ufaransa kwa kuunga mkono utawala wa kijeshi.

Mwezi uliopita kiongozi wa upinzani, Succes Masra, alikuwa imeitaka serikali kueleza ni kwanini mazungumzo ya kitaifa hayakuwa yameanza licha ya kwamba yalistahili kuanza mwezi Mei.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.