Pata taarifa kuu
ANGOLA- TANZIA

Mwili wa Eduardo dos Santos aliyekuwa rais wa Angola umefanyiwa upasuaji.

Mwili wa aliyekuwa rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos, aliyefariki dunia wiki iliyopita, umefanyiwa uchunguzi wa kina baada ya mmoja wa mabinti zake, kuomba hilo akishuku, huenda baba yake aliuawa.

 Aliyekuwa rais wa Angola -Jose Eduardo dos Santos
Aliyekuwa rais wa Angola -Jose Eduardo dos Santos AP - Andre Kosters
Matangazo ya kibiashara

Mawakili wa Welwitschia dos Santos aliyetoa ombi la mwili wa baba yake kufanyiwa uchunguzi huo, wamethibitisha hatua hii lakini hawajatoa majibu.

Ijumaa iliyopita, Mahakama jijini Barcelona iliagiza kufanyika kwa uchunguzi kwenye mwili wa rais huyo wa zamani aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79, baada ya kulazwa hospitalini Juni 23 baaada ya kupata mshtuko wa moyo.

Binti wa rais huyo wa zamani, aliyeongoza Angola kwa zaidi ya miaka 40 amesema kuna dalili kuwa, kifo cha baba yake, hakikuwa cha kawaida.

Mawakili wa famia ya Dos Santos wamehoji ni kwanini mke wake, alitengwa na mgonjwa kwa muda lakini pia kumekuwa na madai ya kiongozi huyo kutoangaliwa vema alipokuwa hospitalini.

Wapinzani wa rais huyo wa zamani wamekuwa wakimkumbuka kama kiongozi aliyetmia utajiri wa mafuta nchini mwake kujitajirisha yeye na familia yake kwa kipindi chote alichokuwa madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.