Burkina Faso : Aliyekuwa rais Blaise Compaore kurejea nyumbani
Aliyekua Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore, ambaye amekuwa uhamishoni nchini Ivyory Coast, tangu mwaka 2014 anatarajiwa kurejea nyumbani kabla ya kumalizika kwa wiki hii.
Imechapishwa:
Ripoti zinasema Compaore, mwenye miaka 71 anatarajiwa kuwasili jijini Ouagadougou, leo au siku ya ijumaa ili kukutana na wakuu wa jeshi katika mkutano wa marais wa zamani.
Rais huyo wa zamani aliyeongoza kwa miaka 27 kaba ya kuondolewa madarakani mwaka 2014 kufuatia maandamano ya wananchi, anarejea nyumbani kufuatia mchakato wa maridhiano ya kitaifa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Compaore ambaye mwezi Aprili alipewa kifungo cha maisha jela kwa kuhusika na rais wa zamani Thomas Sankara, mwaka 1987, akiwa nchini Burkina Faso atapewa makaazi katika nyumba ya serikali, alikokuwa anazuiliwa rais ambaye serikali yake ilipinduliwa na wanajeshi mapema mwaka huu, Roch Marc Christian Kaboré .