Pata taarifa kuu
Nigeria - Siasa

Nigeria : Goodluck Jonathan kuwania urais mwakani

Aliyekuwa rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ametangaza kuwania urais wa taifa hilo na kubadili mpango wa awali wa kutowania, Janathan akiwa miongoni mwa wanasiasa 26 ambao wametangaza nia yao ya kumrithi rais Muhammadu Buhari, ambaye kipindi chake cha kuhudumu kinakamilika mwaka ujao.

 Aliyekuwa rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan
Aliyekuwa rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Jonathan ambaye hivi karibuni ameonekana kuwa mwandani wa karibu wa rais Buhari, amebadili chama chake cha People’s Democratic Party (PDP),  na kujiunga na kile cha rais Buhari All Progressives Congress (APC) ambacho kilimuondoa madarakani mwaka 2015.

Juma lililopita, rais Buhari aliagiza mawaziri wote wanaolenga kuwania nyadhifa za kisiasa kujiuzulu kufikia Mei 16.

Wengine ambao wametangaza kuwania urais ni pamoja na makamo rais wa sasa Yemi Osinbajo, mwenyekiti wa chama tawala Ahmed Bola Tinubu, pamoja na waliokuwa mawaziri 13 na magavana.

Wawaniaji wanaotafuta kupeperusha bendara ya  chama cha upinzani cha PDP, ni pamoja na aliyekuwa makamo rais Atiku Abubakar, aliyekuwa spika wa bunge la seneti Bukola Sarak, gavana wa Sokoto, Aminu Tambuwa na gavana wa jimbo la Rivers Nysom Wike.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.