Pata taarifa kuu
SIASA-KENYA

Kenya: Utata kuhusu uteuzi wa mgombea mwenza katika mrengo wa Odinga

Kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti nchini Kenya, Swala la wagombea wenza bado linaonekana kuwa changamoto kwa wagombea wa urais wakiwemo naibu wa sasa wa rais William Ruto na kinara wa muda mrefu wa upinzani Raila Odinga.

Raila Odinga , Mgombea wa urais kupitia Azimio la Umoja na rais wa sasa Uhuru Kenyatta.
Raila Odinga , Mgombea wa urais kupitia Azimio la Umoja na rais wa sasa Uhuru Kenyatta. © THOMAS MUKOYA/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa Azimio One Kenya, Mrengo anaongoza Raila Odinga , unaendelea na mchakato wa kumtafuta mgombea mwenza baadhi ya majina makubwa katika siasa za taifa hilo la Afrika Mashariki akiwemo Kinara wa chama cha Wiper na aliyewahi kwa wakati moja kuhudumu kama naibu rais  Kalonzo Musyoka.

Elizabeth Meyo , Anayehudumu kama katibu wa jopo linalowapiga msasa wanasiasa waliotuma maombi ya kutaka kuwa wagombea wenza wa mgombea wa urais kwa tiketi ya Azimio One Kenya , Raila Odinga, amethibitisha kuwa wamepokea maombi kutoka wa watu 20 wanaotaka kuwa wagombea wenza wa Odinga.

KANU, mojawapo wa vyama vilivyouunda  muungano huo  umetoa wito wa kuteuliwa kwa Musyoka kama mgombea mwenza wa Odinga.

Nacho chama cha Jubilee kinachoongozwa na rais Kenyatta kimempendekeza mbunge wa zamani wa Peter Kenneth na mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Muranga Sabina Chege kuwa naibu wa Odinga.

Tayari Stephen Kalonzo Musyoka wa wiper amekataa kufika mbele ya jopo linalowapiga msasa watu wanaotaka kuwa wagombea wenza wa Raila Odinga akisema kwamba ndiye anayestahili kuchukua nafasi hiyo.

Jopo hilo lina hadi tarehe 10 ya mwezi mei mwaka huu kumpendekeza mtu anayefaa kuwa mgombea wa Odinga kuelekea tarehe 16 siku ya mwisho ya tume ya uchaguzi nchini humo kupokea majina ya wagombea wenza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.