Pata taarifa kuu

Mali: Jeshi la Ufaransa Barkhane latangaza kukamatwa kwa washukiwa sita Gossi

Ni nini kilifanyika huko Gossi Jumapili hii, Aprili 17, 2022? Vyanzo vya ndani vinashutumu kutekwa nyara kwa wachungaji kadhaa na jeshi la Ufaransa Barkhane ambalo lilikanusha Jumatatu hii na kutoa toleo lake la ukweli.

Doria ya Barkhane huko Gossi nchini Mali.
Doria ya Barkhane huko Gossi nchini Mali. RFI / Olivier Fourt
Matangazo ya kibiashara

Ilikuwa watu watano, wachungaji watano, kulingana na vyanzo vya ndani, "waliotekwa nyara" na kikosi cha Ufaransa Barkhane siku ya Jumapili karibu saa nane usiku huko Adiora. Eneo lililoko takriban kilomita thelathini kaskazini mwa Gossi, huko Gourma-Rharous, katika mkoa wa Timbuktu.

Jeshi la Ufaransa, ambalo liko katika harakati za kujiondoa kutoka eneo hili, lilijibu mara moja habari hii iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii. Kwa mujibu wa maafisa wakuu wa jeshi hilo, operesheni ya kupambana na ugaidi ilifanyika mjini Adiora, usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, ambapo si washukiwa watano, lakini sita walikamatwa.

Mahojiano

"Kwa sasa wanahojiwa na kikosi cha Barkhane", imesema makao makuu ya jeshi, ambayo imebainisha kuwa operesheni hiyo inayozungumziwa ililenga wapiganaji kutoka kundi la Katiba du Gourma, yenye uhusiano na GSIM, Kundi linalotetea Uislamu na Waislamu, wanaohusishwa na al-Qaeda. Na kwamba kundi hili lililengwa kwa kujibu mashambulizi kadhaa yaliyofanywa dhidi ya jeshi la Ufaransa na dhidi ya wakazi wa eneo hilo, bila maelezo zaidi.

Kwa mujibu wa utaratibu unaotumika, washukiwa hao sita, kulingana na hitimisho la mahojiano yao, wataachiliwa au kukabidhiwa kwa mamlaka ya Mali. Jeshi la Ufaransa haliripoti mtu yeyote aliyejeruhiwa au kuuawa, ama upande mmoja au mwingine, wakati wa operesheni hii.

• Barkhane yajiondoa Gossi

Ni mia moja tu kati yao ambao walikuwa bado wamekaa kwenye bonde la Gossi. Jumanne hii saa sita mchana, askari hawa wa mwisho wa Barkhane wameanza kuelekea mji wa Gao. Kambi ya Gossi ilikuwa ikitumika tangu mwezi Septemba 2018.

Kikosi cha Barkhane nchini Mali sasa kiko katika maeneo mawili, kambi kubwa ya mjini Gao kwenye Mto Niger na ile ya Menaka huko Liptako. Kwa upande wao, watarejeshwa kwa Fama ndani ya wiki chache. Mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi yenye silaha hata hivyo yataendelea, hasa kutoka Niger, na kituo cha anga kilichopangwa cha Niamey, lakini kwa idadi ambayo itakuwa nje ya uwiano wowote kwa wale waliotumwa nchini Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.