Pata taarifa kuu
USWISI-HAKI

Algeria: Jenerali Nezzar kuhukumiwa nchini Uswisi

Kesi dhidi ya Khaled Nezzar imedumu muda mrefu kuliko vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Algeria. Mnamo Oktoba 19, 2011, wakati Mkuu huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi akiwa safarini nchini Uswisi, shirika lisilo la kiserikali la Trial iiliwasilisha malalamiko ya jinai dhidi yake katika ofisi ya mashitaka ya Shirikisho (MPC).

Khaled Nezzar katika mkutano na waandishi wa habari huko Paris mnamo 2001.
Khaled Nezzar katika mkutano na waandishi wa habari huko Paris mnamo 2001. THOMAS COEX / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya malalamiko hayo, ofisi ya mashitaka ilifungua uchunguzi kwa "tuhuma za uhalifu wa kivita". Jenerali huyo alikamatwa Oktoba 20, lakini akaachiliwa siku iliyofuata, kwa ahadi ya kuripoti mbele ya ofisi ya mashitaka ikiwa itahitajika.

Kwa mujibu wa ofisi ya mashitaka, MPC, uhalifu ulioshtakiwa ulifanyika "katika mazingira ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Algeria ambavyo, kuanzia maka wa 1992 hadi mwaka wa 1999, vililikuwa kati ya makundi mbalimbali ya Kiislamu dhidi ya serikali".

Mwanaharakati wa mapinduzi ya mwaka1990

Jenerali Khaled Nezzar aliyezaliwa mwaka wa 1937 katika wilaya ya sasa ya Batna, anachukuliwa kuwa mtetezi mkuu wa mapinduzi yaliyokatiza mchakato wa uchaguzi nchini Algeria. Waziri wa Ulinzi kuanzia mwaka wa 1990 hadi mwaka wa 1993, alikuwa mmoja wa wajumbe watano wa Kamati Kuu ya Nchi kuanzia mwaka wa 1992 hadi mwaka wa 1994. Kulingana na shirika hilo lisilo la kiserikali kutoka Uswisii, ambalo linapambana dhidi ya kutoadhibu, "muongo wa giza" ulisababisha watu 200 000 kuuawa au kutoweka kuanzia mwaka wa 1992 hadi mwaka wa 2000. Na Khaled Nezzar alikuwa nambari moja katika utawala wa kijeshi, kiongozi wa kikosi  kilichofanya idadi isiyohesabika ya ukatili". Mnamo mwezi Januari 2012, jenerali huyo alikata rufaa dhidi ya mashtaka yanayomkabili, akibaini kwamba kazi yake kama waziri inamlinda dhidi ya uwezekano wa kufunguliwa mashtaka ya jinai nchini Uswisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.