Pata taarifa kuu

Serikali ya DRC yaombwa kutoa mwanga kuhusu kifo cha Kabagambe aliyeuawa Brazil

Wabunge na mashirika ya kiraia nchini DRC, wameomba serikali ya DRC pomoja na Brazil kutoa mwanga  kuhusu kifo cha raia wa DRC Moïse Kabagambe, ambaye aliuliwa nchini Brazil tarehe  24 Januari , baada ya kupigwa vikali na tajiri wake.

Moïse Kabagambe? mwenye umri wa miaka 24, aliuawa Januari 24 baada ya kupigwa na wanaume watatu katika eneo lake la kazi, ufukweni mwa bahari, katika tukio lilinaswa na kamera za siri.
Moïse Kabagambe? mwenye umri wa miaka 24, aliuawa Januari 24 baada ya kupigwa na wanaume watatu katika eneo lake la kazi, ufukweni mwa bahari, katika tukio lilinaswa na kamera za siri. NELSON ALMEIDA AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati raia kutoka Afrika na Brazil wamefanya maandamano dhidi ya kifo cha Moïse Kabagambe, raia wa DRC aliye fariki huko Brazilia baada ya kupigwa na tajiri wake, nchini DRC hakuna tamko lolote ambalo limetokewa kutoka upande wa mamlaka.

Moïse Kabagambe alikuwa mkimbizi kwa mujibu wa shirika la kiraia katika mkoa wa Ituri, ambapo alikimbia mauaji ya mwaka 2011, Jean-Bosco Lalo kiongozi wa shirika hilo ameomba serikali ya DRC na Brazil kuwadhibu wahusika.

Wizara ya Mambo ya ndani ya DRC imedhibitisha kuwa mazugumzo kati ya serikali hizo mbili, yalianza tu baada ya  taarifa za kifo cha Moïse Kabagambe, huku ikibani kwamba baadhi ya wanashikiliwa na idara husika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.