Pata taarifa kuu

Mkoa wa Tigray waendelea kukumbwa na janga la kibinadamu

Hakuna msafara wa chakula ambao umeweza kufika katika mkoa wa Tigray tangu mwezi Desemba, wakati kulingana na Umoja wa Mataifa, watu 400,000 wanaishi katika mazingira ya njaa. Utawala wa Tigray, unaoshikiliwa na waasi jana ulitoa ripoti kuhusu utapiamlo katika eneo hilo. Njaa tayari imeua zaidi ya watu elfu moja.

Mfanyikazi wa shirika la kutoa msaada la Umoja wa Mataifa huko Addis Ababa, Ethiopia, Aprili 14, 2020.
Mfanyikazi wa shirika la kutoa msaada la Umoja wa Mataifa huko Addis Ababa, Ethiopia, Aprili 14, 2020. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Kati ya mwezi Julai na Oktoba 2021, karibu watu 1,500 wa mkoa wa Tigray walikufa kwa njaa kulingana na ripoti kutoka ofisi ya afya ya mkoa. Takwimu ambazo zilichapishwa na waasi wa Tigray na ambazo haziwezi kuthibitishwa kwa uhuru.

Kwa jumla, zaidi ya watu 5,400 walibeba mzigo mkubwa wa mgogoro wa kibinadamu, ukosefu wa dawa. Waathirika hasa wa njaa, lakini pia magonjwa ya kuambukiza.

Mwaka jana, 15% tu ya misaada muhimu iliweza kuingia Tigray. Vizuizi vya misaada kwa wakaazi wa mkoa huo vilivyowekwa na serikali ya Ethiopia viliimarishwa zaidi mwishoni mwa mwaka jana. Hakuna msaada wowote ulioweza kusafirishwa katika mkoa wa Tigray tangu Desemba 15.

Ili kuhalalisha hatua ya kuweka kizuizi chake, serikali inawashutumu waasi wa Tigray kwa kupora misaada au kushambulia misafara. Vikosi vya Ulinzi vya Tigray vinaishutumu Addis Ababa kwa kutaka kukomesha eneo hilo kimakusudi.

Msafara wa mwisho, ambao ulikuwa wa kubeba tani 800 za chakula hadi mkoa wa Tigray, ulifutwa katika dakika za mwisho siku ya Jumatatu huku mapigano yakizuka kwenye barabara pekee inayotumiwa kwa kusafirisha msaada kuelekea eneo hilo.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kujadili leo, kwa mara nyingine, hali ya kibinadamu huko Tigray.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.