Pata taarifa kuu

DRC: Timu ya Tume Huru ya Uchaguzi yakamilika

Miezi kadhaa baada ya kuidhinishwa na Bunge la kitaifa, Mahakama ya kikatiba nchini DRC, imeridhia kiapo cha wajumbe watatu wa upinzani kutoka muungano wa FCC katika Tume Huru ya Uchaguzi, CENI, ambayo sasa imekamilika.

Mbele ya makao makuu ya Tume Huru ya Uchaguzi (CENI), Novemba 5, 2017 huko Kinshasa.
Mbele ya makao makuu ya Tume Huru ya Uchaguzi (CENI), Novemba 5, 2017 huko Kinshasa. JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja baada ya wajumbe hao kutoka muungano wa FCC chini ya rais wa zamani Joseph Kabila kuungana na tume hiyo ya uchaguzi, CENI, licha ya kutokubaliana na wajumbe wengine kutoka muungano huo.

Wajumbe hao ambao ni mbunge Didier Manara ambaye amekula kiapo kama makamu wa pili wa rais, Agée Matembo kama mratibu na Jean Ilongo kama mjumbe wa kikao baada ya majadiliano makali ndani ya jukwaa la wanasiasa walio upande wa rais wa zamani wa nchi hiyo, ambao mwanzoni walionekana kupinga uteuzi wa Mwenyekiti wa sasa wa tume hiyo Denis Kadima.

Kwa upande wake kiongozi wa vuguvugu ndani ya FCC Nogec Constant Mutamba amesema Kabila ni falsafa, haifai kumzungumzia katika mambo ya chini, na kwamba wameungana na Tume Huru ya Uchaguzi kama kuhakikisha wazo la kiongozi huyo ambaye anataka kuuona mchakato wa Uchaguzi nchini DRC unapiga hatua .

Kulingana na Marie Ange Mushobekwa , msemaji wa tume ya dharura kutatua mzozo ndani ya FCC, wataendelea kupambana kuhakikisha sheria ya uchaguzi itayopigiwa kura hivi karibuni inatoa dhamana ya uchaguzi huru na wa haki.

Wakati huo huo Jean-Marc Kabund ametangaza kujiuzulu kama naibu spika wa Bunge la taifa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kabund amesema amefikia uamuzi wa kuachia nafasi hiyo kwa kile alichokieleza ni hatua inayokuja baada ya kudhalilishwa na kuteswa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.