Pata taarifa kuu

Chanjo kwa watoto wa miaka 12-17 yaanza Guinea

Ijumaa wiki hii, katika mikoa ya Conakry na Kindia, chanjo ya vijana wenye umri wa miaka 12 hadi 17 dhidi ya Covid-19 ilianza. Hadi Januari 21, timu za wahudumu wa afya zitatembelea shule hasa. Lengo: Kufikia chanjo kamili ya angalau 85% ya vijana katika maeneo haya mwishoni mwa mwezi Februari.

Vijana wakipita mbele ya mabango yanayohimiza watu kuchanjwa dhidi ya Covid-19.
Vijana wakipita mbele ya mabango yanayohimiza watu kuchanjwa dhidi ya Covid-19. CELLOU BINANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza kwa kampeni ya chanjo kuwalenga vijana nchini Guinea, nchi ambayo inakabiliwa na mlipuko wa maambukizi wa virusi vya covid-19. Uchunguzi ulibainisha mwishoni mwa mwezi Desemba kwamba kirusi kipya cha Omicron kilikuwa kikisambaa huko Conakry.

Viongozi wa shule wameonekana wakihamasisha wanafunzoi wao kuitiki chanjo kwa wingi ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona, hususan katika shule ya Mohamed Lamine Sidibé, nje kidogo ya mji mkuu. "Nyote mtachanjwa, mmoja baada ya mwingine, msiwe na haraka, polepole! Mkuu wa shule Mamadou Bah amekuwa akiwaambia wanafunzi wake, huku akijaribu kutuliza kidogo taharuki iliyozuka kufuatia wanafunzi kutilia mashaka chanjo hiyo inayotolewa kwa watu wengi kwa wakati mmoja.

"Tunahamasisha kila asubuhi kabla ya kuanza visomo na wanafunzi wamefaulu kuwashawishi wazazi wao kukubali chanjo hii kama unavyoona. Hapo awali watu walikuwa wakikimbia, lakini hivi sasa mambo yamebadilika, hivi wanaitikia kwa wingi. Ujumbe huo ulipitishwa kwa familia na mambo yanaendelea vizuri, "amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.