Pata taarifa kuu
NIGER-HAKI

Niger: Serikali yajieleza kuhusu kesi ya ubadhirifu katika Ulinzi

Video ilirushwa Alhamisi hii, Januari 6, 2022, kwenye ukurasa wa  Twitter ya ofisi ya rais. Ukaguzi wa matumizi ya fedha uliofanywa na Wizara ya Ulinzi ulifichua mwaka wa 2020 kwamba makumi ya mabilioni ya faranga za CFA yalielekezwa kinyume "kupitia" malipo ya ziada, ankara za uwongo au maagizo ambayo hayajawasilishwa. Kwa hivyo, Wakala wa Mahakama wa serikali alikuwa lianzisha kesi za kisheria.

Wanajeshi wa Niger wakishika doria pembezoni mwa mji wa Bosso, katika eneo la Diffa, Mei 25, 2015.
Wanajeshi wa Niger wakishika doria pembezoni mwa mji wa Bosso, katika eneo la Diffa, Mei 25, 2015. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, agizo la mkuu wa majaji hao lilifichua kwamba serikali hatimaye imeacha kuchukua hatua zake za kisheria kufuatia mazungumzo ambayo yaliiwezesha kurejesha pesa zilizofujwa. Uamuzi ambao uliamsha hasira kwa sehemu za mashirika ya kiraia na upinzani.

Ufafanuzi

Baada ya ukimya wa siku kadhaa, serikali imetaka kufafanua msimamo wake. Kutokana na kurejeshwa kwa fedha hizo, kipengele cha kiraia cha utaratibu wa kisheria kimekamilika, kulingana na Tidjani Idrissa Abdoulkadri, msemaji wa serikali: "Hizi bilioni 12 zimepatikana na kwa hivyo, kinyume na utaratibu, Serikali haijaweka utaratibu utakaotosheleza pande zote katika kesi hi. Kwa hiyo hakuna nia ya serikali kusimamisha kesi hiyo. Kinyume na inavyoaminika, ni serikali inayopaswa kupongezwa kwa nia yake ya kusafisha na kupambana na ufisadi na ubadhirifu wa aina yoyote. "

Baadhi walikasirishwa nchini Niger kwa kutoona washukiwa wakifunguliwa mashtaka kwa makosa yao. Msemaji wa serikali anakumbusha kwamba kesi za jinai bado hazijakamilika: "Taarifa hii haimaanishi kuwa kesi za kisheria zimesimamishwa. Kinyume chake, kesi bado iko mahakamani na utaratibu utafuata mkondo wake. Na wale ambao wanahusika watakuwa chini ya uamuzi wa mahakama. Suala la kesi ni suala la haki. Tuko kwenye demokrasia yenye mgawanyo wa wazi wa madaraka na mahakama itashughulikia suala hilo ipasavyo. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.