Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Mpatanishi wa ECOWAS: Kipindi cha mpito cha miaka 5 nchini Mali hakiwezekani

Goodluck Jonathan, mpatanishi wa Jumuiya ya Nchi za Kiuchumi za Afrika Magharibi, ECOWAS, alikuwa katika ziara nchini Mali ya kuwasilisha ujumbe kutoka kwa wakuu wa nchi wa jumuiya hiyo kwa rais wa mpito, Kanali Assimi Goïta. Ziara hii pia ni hatua muhimu kabla ya mkutano usio kuwa wa kawaida wa wakuu wa nchi za ECOWAS utakaofanyika Januari 9.

Rais wa zamani Goodluck Jonathan, mpatanishi wa ECOWAS katika mzozo wa Mali, wakati wa ziara ya hivi karibuni nchini Mali.
Rais wa zamani Goodluck Jonathan, mpatanishi wa ECOWAS katika mzozo wa Mali, wakati wa ziara ya hivi karibuni nchini Mali. REUTERS - AMADOU KEITA
Matangazo ya kibiashara

Mkutano kati ya rais wa mpito, Kanali Assimi Goïta na mwakilishi wa ECOWAS, Goodluck Jonathan, ulitarajiwa na ulidumu kwa karibu saa mbili katika ikulu ya rais huko Koulouba. Mwishoni mwa mkutano huu, rais wa zamani wa Nigeria pamoja na ikulu ya rais wa Mali hawakutaka kuzungumza chochote kuhusiana na mazungumzo yao.

Ikulu ya rais wa Mali, imeandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba kuna maendeleo katika hali ya kisiasa nchini Mali, kulingana na mwandishi wetu wa habari huko Bamako, Kaourou Magassa. Katika mazungumzo yao, hata hivyo, kulikuwa na suala la ratiba iliyopendekezwa kuhusu kipindi cha mpito kiongezwe kwa miaka mitano.

Wakati wa mkutano na mabalozi wa nchi za kigeni nchini Mali na wajumbe wa ECOWAS, pendekezo hili lilikataliwa na viongozi wengi walioshiriki mkutano huo. Pia vyama kadhaa vya siasa na mashirka ya kiraia ambavyo wakati huo huo viliandaa mkutano na waandishi wa habari vilibaini kwamba havikubaliani na pendekezo hilo.

Kwa mujibu wa wanadiplomasia wa nchi za kigeni huko Bamako, Goodluck Jonathan amebaini wazi kuwa kipindi cha mpito cha miaka mitano kilichopendekezwa na serikali ya Mali hakiwezekani. Mjumbe wa ujumbe wa upatanishi aliongeza mbele ya waandishi wa habari: "Miaka mitano ya kipindi cha mpito kwa watu waliopindua serikali? Ni, kwa mfano, zaidi ya muhula wa rais aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Nigeria ".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.