Pata taarifa kuu

Nchi za Kiafrika zakabiliwa na mzozo wa kiuchumi unaohusishwa na Covid-19

Mwaka 2021 ulikumbwa tena na janga la Covid-19 na mlolongo vizuizi ambavyo vimekuwa na athari kubwa kwa uchumi wa ulimwengu na vile vile barani Afrika. Kwa mwaka mpya, matangazo ya hatua za kudhibiti mfumuko wa bei na kupunguza athari kwa raia yameongezeka.

Mji mjuu wa Togo, Lomé.
Mji mjuu wa Togo, Lomé. AFP - YANICK FOLLY
Matangazo ya kibiashara

"Kufunguliwa tena kwa uchumi" ni kile Rais wa Uganda Yoweri Museveni alitangaza Ijumaa jioni katika hotuba yake ya Mwaka Mpya. Pamoja na kufunguliwa tena kwa sekta ya uchukuzi, sinema, kumbi za michezo, shule za msingi na sekondari… Hadi mwisho wa mwezi Januari sheria ya kutotoka nje. inaweza kuondolewa, isipokuwa kwa pikipiki za kukodiwa.

Nchini Togo, malipo ya awali ya mshahara wa mwezi mmoja kwa watumishi wa umma; "hayua kali ya kudhibiti bei," na malipo ya fidia sawa na mishahara ya miezi mitatu kwa watu waliostaafu. Hizi hapa ni hatua za kupambana na gharama ya juu ya maisha zilizowasilishwa na Rais Faure Gnassingbe wakati wa hotuba yake Mwaka Mpya.

Mapema wiki hii nchini Chad, rais wa CNT aliahidi juhudi kwa vijana: pamoja na mambo mengine, kuinguzwa kwa vijana 5,000 katika utumishi wa umma mwaka 2022, vifaa kwa makampuni ambayo yataajiri vijana, au kupungua kwa 30% kwa gharama ya upatikanaji wa intaneti katika robo ya kwanza.

Rwanda, nchi adimu iliyo katika hali nzuri

Nchini Benin, Rais Talon katika hotuba yake kwa Bunge la taifa wiki hii aliangazia mapambano dhidi ya Covid-19. "Sisi ni waathiriwa wa hali inayojiri kwa sasa duniani na ni vita vya ushindi dhidi ya janga hili ambayo itasaidia sana kurudisha nyuma hali hii kuelekea gharama kubwa ya maisha," alisema.

Nchini Tunisia, Alhamisi katika Baraza la Mawaziri. "Ugavi wa vifaa muhimu na udhibiti wa bei" ni suala ambalo lilikuwa kwenye ajenda.

Hakuna hatua mpya katika hotuba ya Mwaka Mpya ya rais wa Rwanda. Lakini niwashukuru wananchi kwa bidii yao katika nyakati hizi ngumu. Paul Kagame alitoa mojawapo ya ripoti chache nzuri na ukuaji "mkubwa" wa uchumi nchini Rwanda mwaka 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.