Pata taarifa kuu

Umoja wa Afrika na Somalia kutathmini hatima ya AMISOM

Somalia na Umoja wa Afrika zimekubaliana kuthathmini operesheni za jeshi la AMISOM, ambalo muda wake uliongezwa mpaka mwezi Machi mwaka 2022.

Kikosi cha wanajeshi wa Burundi walioko Somalia chini ya uongozi wa AMISIOM, mjini Mogadishu tarehe 11 Julai 2017.
Kikosi cha wanajeshi wa Burundi walioko Somalia chini ya uongozi wa AMISIOM, mjini Mogadishu tarehe 11 Julai 2017. © AFP / Mohamed Abdiwahad
Matangazo ya kibiashara

Katika kikao cha pamoja, kati ya serikali ya Somalia, na wawakilishi wa Umoja wa Afrika, wamekubaliana kuanza majadialiano kuhusu hatima ya AMISOM, kuanzia Januari, majadiliano ambayo ambayo yanatarajiwa kudumu kwa siku 30.

Miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa na pande hizo mbili ni pamoja na namna ya kufadhili operesheni hiyo na namna ya kuendeleza mapambano dhidi ya kundi la Al Shabab na makundi mengine ya kigaidi nchini Somalia.

Baada ya majadiliano hayo, pande zote zinatarajiwa kuwasilisha ripoti yake kwa Tume ya amani na usalama ya Umoja wa Afrika, kuanzia Februari 11 mwaka 2022.

Ni wiki iliyopita tu ambapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliongeza muda wa AMISOM kusalia nchini Somalia kwa kipindi cha miezi mitatu zaidi, wakati huu Barzala la uysalama la Umoja, Afrika linapotarajiwa kupendekeza kikosi hicho kusalia nchini humo mpaka 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.