Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Mkuu wa MONUSCO: Hali ya usalama bado ni tete katika mkoa wa Kivu Kusini

Siku chache kabla ya kumalizika kwa muhula wake kwa mwaka huu, ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unaona kuwa hali ya usalama bado ni tete katika mkoa wa Kivu Kusini licha ya juhudi zinazofanywa.

Gari la MONUSCO huko Kivu Kusini.
Gari la MONUSCO huko Kivu Kusini. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa huko Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, mkuu wa ofisi ya MONUSCO katika mkoa huo alirelea juhudi hizi, na changamoto za mwaka 2021.

Karna Soro alianza kwa kukaribisha maendeleo kwa ushirikiano kati ya MONUSCO, jeshi, polisi na mamlaka ya kisiasa na utawala. "Sisi, pamoja na mamlaka, tuliwarejesha katika maisha ya kiraia wapiganaji 211, raia wa DRC, na wapiganaji 40 wa kigeni waliorejeshwa makwao, wengi wao ambao ni kutoka kundi la zamani la waasi wa Kihutu la FDLR walirudi Rwanda. Tulipokonya zaidi ya silaha 60 zinazofanya kazi. Makundi manne yenye silaha yamesambaratishwa: Maheshe, Ndarumanga, Bralima, Mabuli, haya ni makundi ambayo hayapo tena,” alieleza.

Mengi ya kufanywa

Mkuu wa ofisi ya MONUSCO huko Bukavu pia alisifu juhudi za upatanishi za kuishi pamoja kwa amani huko Kalehe, Minembwe, na Uvira, lakini aalibaini kuwa bado kuna mengi ya kufanywa.

“Kwa bahati mbaya kuna baadhi ya maeneo kama vile nyanda za juu za Uvira ambako mivutano inaendelea kati ya jamii, ambapo bado tuna idadi kubwa ya watu waliokimbia makazi yao ingawa tunaweza kusema kwamba katika maeneo haya pia tumesaidia watu kuzungumza wao kwa wao , aliongeza. Hivi majuzi waliohama kutoka Bibokoboko walirudi kwa msaada wa FARDC kwa ushirikiano na MONUSCO, tunashirikiana na washirika wetu wa FAO kuwarudisha wakimbizi wa ndani kutoka Bijombo.Tumesambaza nafaka za chakula katika eneo la Mikenge. Kuna juhudi zinazofanywa lakini changamoto zinabaki kuwa katika maeneo kadhaa suala la kuishi pamoja kwa amani linabaki kuwa tete. "

Vituo saba vya mafunzo

MONUSCO huko Kivu Kusini imeanzisha vituo saba vya mafunzo kwa biashara tofauti ili kuwashughulikia wapiganaji wanaokubali kuweka chini silaha zao kama sehemu ya mpango wa kuwapokonya silaha, kuwarejesha katika maisha ya kraia na kuwaunganisha tena na jamii zao, mpango ulioanzishwa hivi karibuni na Rais Félix Tshisekedi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.