Pata taarifa kuu
UTURUKI-USHIRIKIANO

Uturuki yakutana na viongozi kadhaa wa Afrika kwa minajaili ya kuboresha ushirikiano

Mkutano wa tatu wa ushirikiano  kati ya mataifa ya bara la Afrika na Uturuki, umeanza jijini Instanbul, ambapo viongozi na Mawaziri kutoka mataifa 39 wanahudhuria.

Baada ya ziara yake barani Afrika, Rais Recep Tayyip Erdogan anapokea viongozi wa Afrika wakati wa mkutano wa 3 wa kilele wa Afrika na Uturuki.
Baada ya ziara yake barani Afrika, Rais Recep Tayyip Erdogan anapokea viongozi wa Afrika wakati wa mkutano wa 3 wa kilele wa Afrika na Uturuki. Osvaldo Silva AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu wa siku mbili unafanyika baada ya kuahirishwa mara mbili kwa sababu ya janga la Covid-19.

Uturuki inasema, lengo kuu la mkutano huu ni kuimarisha uhusiano kati yake na mataifa ya Afrika katika masuala hasa ya biashara , usalama, na kilimo.

Rais Recep Tayyip Erdogan anasema lengo la serikali yake ni kuongeza kiwango cha kufanya biashara kati ya nchi yake kufika Dola Bilioni 50, wakati huu Shirika la ndege la Uturuki, lilifanya safari katika nchi 28 barani Afrika.

Suala la ushirikiano wa kiusalama ni muhimu katika mkutano huu, wakati huu Uturuki ikiwa na kambi ya kijeshi nchini Somalia, lakini pia imekuwa ikituma vikosi vyake nchini Libya na imekuwa ikiyauzia mataifa ya Afrika, vifaa vya kijeshi hasa mataifa ya Ethiopia, Angola, Chad na Morocco.

Wanadiplomasia na wachambuzi wa mambo wanasema, rais Erdogan anaonekana kupata uungwaji mkono kutoka kwa viongpzi wa Afrika, baada ya kutofautiana na viongzi wa nchi za Magharibi kuhusu namna wanavyoshirikiana na mataifa ya Afrika, huku yeye akichukua msimamo wa kutoonesha ubaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.