Pata taarifa kuu
GAMBIA-UCHAGUZI

Gambia yafanya uchaguzi wa kihistoria

Zaidi ya raia 960,000 wa Gambia wanapiga kura kumchagua rais wao mpya Jumamosi hii, Desemba ikiwa ni uchaguzi wa kwanza wa urais tangu Yahya Jammeh kushindwa 2016, baada ya miongo miwili ya utawala wa kimabavu.

Nchini Gambia, muungano wa mashirika ya kiraia, na Wanep, unatuma waangalizi 150 kwa ajili ya uchaguzi wa urais mnamo Desemba 4, 2021.
Nchini Gambia, muungano wa mashirika ya kiraia, na Wanep, unatuma waangalizi 150 kwa ajili ya uchaguzi wa urais mnamo Desemba 4, 2021. © RFI/Paulina Zidi
Matangazo ya kibiashara

Wagombea sita wanashiriki kwenye kinyang'anyiro hicho, akiwemo rais anayemaliza muda wake Adama Barrow na makamu wake wa zamani Ousainou Darboe, mpinzani wa kihistoria.

Uchaguzi huu unachukuliwa kuwa "jaribio" kwa demokrasia hii changa ambao unafanyika chini ya uangalizi wa waangalizi wa kitaifa na kimataifa.

Rais wa sasa Adama Barrow aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2016, ana matumaini ya kushinda muhula wa pili

Wagombea sita wanagombea kiti cha urais. Wachambuzi wanasema ushindani mkali ni kati ya wagombea wawili ambao ni Rais Adama Barrow wa chama cha NPP na aliyekuwa Naibu wake Ousainou Darboe anayegombea kwa tiketi ya chama cha United Democratic Party (UDP).

Gambia ni nchi changa kidemokrasia inakabiliwa na changamoto chungu nzima, kuanzia ukosefu wa ajira hasa miongoni mwa vijana, masuala ya afya, elimu, miundombinu, na uchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.