Pata taarifa kuu
DRC-MAENDELEO

DRC: Bunge la Seneti kujadili na mabunge ya majimbo kuhusu masuala tete

Bunge la Seneti nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo limeweka mfumo wa mazungumzo na mashauriano na mabunge ya majimbo. Lengo ni kuboresha utawala wa taasisi za mitaa. Mpango unaoongozwa na rais wa Bunge la Seneti, Modeste Bahati Lukwebo.

Makao makuu ya Baraza la Wawakilisi na Bunge la Seneti.
Makao makuu ya Baraza la Wawakilisi na Bunge la Seneti. © Junior D.Kannah/AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku nne za tafakuri kati ya maseneta, maspika wa mabaraza ya majimbo na wakuu wa tawala za majimbo 26 ya nchi zimepelekea kuanzishwa kwa mfumo huo.

Ni lazima kuhakikishwe utawala bora wa majimbo na, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, jukumu hili ni la Bunge la Seneti, amesema Modeste Bahati Lukwebo.

Kwa upande wa rais wa Bunge la Seneti, kanuni za ndani za Bunge la Seneti zinatoa mfumo wa mazungumzo na mashauriano na mabunge ya mkoa. "Kwa hivyo, tuliona kuwa ni muhimu kurasimisha mfumo huu, ili mara kwa mara tuweze kukutana kwanza kubadilishana uzoefu. Pili, kutathmini hali inavyoendelea mikoani. Na unajua, katika miezi ya hivi karibuni, kumekuwa na machafuko mengi katika majimbo… ”

Mfumo huu wa mashauriano utakuwa ukifanyika mara moja au mbili kwa mwaka ili kuimarisha utawala wa taasisi zilizopewa majukumu na kujitawala, amebaini Bahati Lukwebo. Miongoni mwa masuala yatakayotatuliwa ni pamoja na yale ya kodi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.