Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-HAKI

Sierra Leone: Mwanasiasa anayepinga ufisadi Lara Taylor-Pearce asimamishwa kazi

Mkaguzi mkuu Lara Taylor-Pearce, kiongozi anayesifiwa katika vita dhidi ya ufisadi kwa miaka kadhaa nchini Sierra Leone, amesimamishwa kazi na serikali. Uamuzi "usioelezeka" wiki chache tu kabla ya kuchapishwa kwa ripoti inayotarajiwa juu ya usimamizi wa fedha za umma na serikali ya Sierra Leone mwaka 2020.

Tangazo la kusimamishwa kazi kwa Lara Taylor-Pierce, Alhamisi hii, Novemba 11, liliishangaza wengi nchini Sierra Leone.
Tangazo la kusimamishwa kazi kwa Lara Taylor-Pierce, Alhamisi hii, Novemba 11, liliishangaza wengi nchini Sierra Leone. Mohamed Saidu Bah
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la kusimamishwa kazi kwa Lara Taylor-Pierce, Alhamisi hii, Novemba 11, liliishangaza wengi nchini Sierra Leone. Kiongozi mkweli katika vita dhidi ya ufisadi kwa zaidi ya miaka kumi na mkaguzii mkuu alipokea barua kuachiswhwa kazi siku ya Alhamisi. Lara Taylor-Pearce na msaidizi wake wamesimamishwa kazi mara moja. Pia amepata taarifa kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaunda mahakama ya kuchunguza kazi ya idara yake ya ukaguzi.

Hakuna maelezo

Hakuna maelezo, ni mshangao kwa wasaidizi wake na katika upande wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayopambana na ufisadi, ambao hawaelewi uamuzi huu. "Sijaambiwa majukumu ya mahakama hii ni  au ni kitendo gani cha kulaumiwa tulifanya" amelaumu Lara Taylor-Pearce, ambaye anakanusha kabisa makosa ya aina yoyote katika utekelezaji wa mamlaka yake.

Kusimamishwa huku kulizua hisia nyingi nchini Sierra Leone, kwani uamzi huu unakuja wiki chache tu kabla ya kuchapishwa kwa ripoti ya usimamizi wa fedha za umma. Lara Taylor-Pearce anajulikana sana kwa kutumia miaka kumi iliyopita kukagua akaunti za umma za nchi, na kwa kufichua visa vingi vya udanganyifu wakati wa mgogoro wa afya uliosababishwa na ugonja wa Ebola mnamo mwaka 2014 na 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.