Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-USALAMA

Takriban watu 80 wafariki katika mlipuko wa bohari ya mafuta Freetown

Mlipuko wa bohari ya mafuta umeua takriban watu 80 katika eneo la viwanda la Freetown, mji mkuu wa Sierra Leone, huko Afrika Magharibi. "Tulipata miili 80 kutoka eneo la ajali jana usiku," afisa wa shirika la Msalaba Mwekundu amesema, akiongeza kuwa shughuli za kutoa misaada zimekuwa zikiendelea leo Jumamosi asubuhi (Novemba 6).

Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio, ambaye yuko nchini Scotland Jumamosi hii kuhudhuria mazungumzo ya tabia nchi yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa amesema, anahuzunishwa "kuwapoteza raia wote hao ambao wengi wamefariki katika mazingira mabaya".
Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio, ambaye yuko nchini Scotland Jumamosi hii kuhudhuria mazungumzo ya tabia nchi yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa amesema, anahuzunishwa "kuwapoteza raia wote hao ambao wengi wamefariki katika mazingira mabaya". Marimé BRUNENGO AFP
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ulisababishwa na gari lililoshika moto katika kituo cha mafuta kufuatia ajali ya barabarani, walioshuhudia wamesema.

Muuguzi mmoja katika hospitali ambayo waathiriwa walipelekwa amethibitisha idadi ya vifo kwa Shirika la Habari la AFP, pia akisema kuwa amepokea wanawake wengi, wanaume na watoto na wakiwa na "majeraha mabaya".

Mlipuko huo ulisababishwa na gari lililoshika moto katika kituo cha mafuta kufuatia ajali ya barabarani, mashuhuda wamesema, na moto huo ukasambaa katika eneo hilo. Miili kadhaa iliyoteketea kwa moto ilipatikana katika magari na mitaa ya karibu. Kulingana na Shirika la Habari la Associated Press, wakaazi walikuwa wamekusanyika katika eneo hilo ili kupata mafuta yaliyomwagika.

Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio, ambaye yuko nchini Scotland Jumamosi hii kuhudhuria mazungumzo ya tabia nchi yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa amesema, anahuzunishwa "kuwapoteza raia wote hao ambao wengi wamefariki katika mazingira mabaya". "Rambirambi zangu za dhati kwa familia ambazo zimepoteza wapendwa wao ," ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter. Makamu wa Rais Mohamed Juldeh Jalloh amezuru eneo hilo Jumamosi asubuhi, akiambatanana ujumbe wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.