Pata taarifa kuu

Baada ya mzozo wa nyambizi, Macron na Biden kukutana Roma

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Marekani Joe Biden watakutana leo jioni, Oktoba 29, huko Roma kabla ya ufunguzi wa mkutano wa mataifa yaliyostawi kiuchumi, G20, ambayo viongozi hao wawili watashiriki katika mji mkuu wa Italia.

Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe, Jill Biden, wakishuka kutoka kwenye ndege ya "Air Force One" walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rome Fiumicino mapema Oktoba 29, 2021, mjini Rome, Italia.
Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe, Jill Biden, wakishuka kutoka kwenye ndege ya "Air Force One" walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rome Fiumicino mapema Oktoba 29, 2021, mjini Rome, Italia. AFP - BRENDAN SMIALOWSKI
Matangazo ya kibiashara

Mkutano ambao unatarajia kukamilisha maridhiano kati ya Ufaransa na Marekani baada ya mzozo uliosababishwa na uamuzi wa Australia kuvunja mkataba wa ununuzi wa nyambizi za Ufaransa, kwa manufaa ya Marekani.

Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Villa Bonaparte, kwenye Ubalozi wa Ufaransa. Emmanuel Macron ndye atampokea mwenzake wa Marekani. kulingana na rais wa Jamhuri, hii ina umuhimu wa kiishara na kisiasa, ameripoti mwandishi wetu maalum huko Roma, Valérie Gas.

Njia moja ya kuonyesha kuwa Joe Biden anakuja kugeuza ukurasa juu ya shida iliyosababishwa na kile Ufaransa ilikuwa imeelezea kama "usaliti" wa mshirika wake Marekani. Kwa mara ya kwanza katika historia, balozi wa Ufaransa nchini Marekani alikuwa amerudishwa nyumbani jijini Paris.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.