Pata taarifa kuu

Joe Biden na Emmanuel Macron kukutana Roma siku ya Ijumaa

Ikulu ya White House imesema viongozi hao wawili watakutana tarehe 29 Oktoba, kabla tu ya mkutano wa kilele wa G20 katika mji mkuu wa Italia, Roma.

Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano wa kilele wa G7 huko Carbis, Uingereza Juni 13, 2021.
Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano wa kilele wa G7 huko Carbis, Uingereza Juni 13, 2021. AFP - DOUG MILLS
Matangazo ya kibiashara

Itakuwa mara ya kwanza kwa Emmanuel Macron na Joe Biden kukutana tangu mzozo wa nyambizi ya Australia. Mkutano kati ya rais wa Ufaransa na mwenzake wa Marekani umepangwa kufanyika Ijumaa, Oktoba 29, mjini Roma, kabla ya mkutano wa kilele wa G20.

Tangazo hilo limetolewa Jumanne na mshauri wa usalama wa kitaifa wa Ikulu ya White House Jake Sullivan, bila kutoa maelezo zaidi. Tangu kutangazwa kwa muungano mpya kati ya Washington, Canberra na London katikati ya mwezi wa Septemba dhidi ya Paris, uhusiano kati ya Ufaransa na Marekani haujakuwa katika hali nzuri.

Ushirikiano huu, uliopewa jina la Aukus, uliamsha hasira adimu kutoka Ufaransa, kwa sababu ulivunja mkataba mkubwa wa nyambizi ulioafikiwa kati ya Ufaransa na Australia. Tangu wakati huo, Washington imekuwa ikijaribu kurekebisha mambo. Joe Biden na Emmanuel Macron tayari wamezungumza kwa simu mara mbili tangu mzozo huo kuzuka. Aidha, Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris atazuru Paris mwezi Novemba.

Mkutano na Papa Francis juu ya mpango wa Joe Biden

Ufaransa inatafuta hasa kupata baraka za Marekani kwa ajili ya kuunda ulinzi halisi wa Ulaya, mradi muhimu kwa Ufaransa lakini ambao bado haujachukua sura nzuri miaka 30 baada ya kuzinduliwa kwake.

Joe Biden pia atakutana kwa mazungumzo na Papa Francis na mkuu wa serikali ya Italia Mario Draghi siku ya Ijumaa, Jake Sullivan amesema. Hata hivyo, hakuelezea mikutano mingine ya nchi mbili ambayo rais wa Marekani anaweza kufanya huko Roma na kisha Glasgow, ambako atashiriki katika mkutano wa kimataifa wa tabianchi, COP26.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.