Pata taarifa kuu
MALI-SIASA

Mali: Baraza la Usalama la UN ziarani Bamako

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unafanya ziara nchini Mali Jumamosi, Oktoba 23 alasiri. Ikiwa ni ziara ya kikazi ya siku mbili ambayo ni sehemu ya mashauriano ya kawaida kati ya serikali ya Mali na Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwa Tume ya Umoja huo nchini Mali, MINUSMA, mnamo mwaka 2013.

Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali, (MINUSMA) wako nchini humo tangu mwaka 2013.
Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali, (MINUSMA) wako nchini humo tangu mwaka 2013. AFP/Sebastien Rieussec
Matangazo ya kibiashara

Lakini ziara hii inakuja katika hali ya mvutano kati ya Bamako na washirika wake wa kimataifa juu ya uwezekano wa mkataba na mamluki wa Urusi kutoka kampuni ya Wagner, na hasa juu ya upanuzi wa uwezekano wa kipindi cha mpito. Mamlaka walijikubalisha kuhudumu kwa kipindi cha miezi 18 lakini sasa wanafikiria kusogeza mbele kipindi hiki.

Ujumbe wa Baraza la Usalama unaongozwa na Kenya, inayoongoza Baraza la Usalama la Imoja aw Mataida mwezi huu wa Oktoba, Niger na Ufaransa. Ujumbe huu unatarajiwa kukutana na wawakilishi wa serikali ya Mali na rais wa Mpito, Kanali Assimi Goïta, lakini pia, kulingana na chanzo cha Umoja wa Mataifa, na makundi yenye silaha yaliyo tia saini kwenye makubaliano ya amani ya mwaka 2015 na mashirika ya kiraia.

Kwa upande wake, wizara ya mambo ya nje ya Mali inabainisha kuwa "lengo kuu la ujumbe huu ni kutathmini hali ya kisiasa, usalama na haliya kibinadamu", na pia kuheshimu haki za binadamu nchini..

Baada ya ziara hii nchini Mali, ujumbe wa Umoja wa Mataifa utakwenda Niamey, mji mkuu wa Niger Jumapili Alaasiri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.