Pata taarifa kuu
SAHEL-USHIRIKIANO

G5 Sahel yazindua mpango wa kupunguza umaskini katika eneo la mipaka 3

Nchini Mauritania, mpango wa kufadhili miradi ya kijamii kwa manufaa ya raia walio katika mazingira magumu katika ukanda wa G5 Sahel ulizinduliwa Alhamisi hii, Oktoba 21, 2021, katika makao makuu ya jumuiya hiyo huko Nouakchott.

Sekretarieti ya Kudumu ya G5 Sahel huko Nouakchott nchini Mauritania.
Sekretarieti ya Kudumu ya G5 Sahel huko Nouakchott nchini Mauritania. RFI/Paulina Zidi
Matangazo ya kibiashara

Ufadhili huu kutoka kwa serikali ya Ujerumani ndani ya mfumo wa G5 Sahel kimsingi unalenga waathiriwa wa ugaidi katika eneo la Liptako-Gourma, linalojulikana kama eneo la mipaka mitatu, Burkina-Mali-Niger. Eneo ambalo uwepo wa makundi ya kigaidi huongeza umaskini na ukosefu wa usalama.

Zoezi la kwanza la mpango huo litaanza katika mkoa wa Mali wa Gao kabla ya mwisho wa mwaka. Mali ni moja wapo ya nchi zilizoathiriwa zaidi na umasikini unaotokana na mgogoro wa usalama ambao unaukumba ukanda wa Sahel tangu mwaka 2012.

"Hili ndilo eneo leo ambapo kunapatikana wanyonge zaidi, ambapo raia wanakabiliwana mahitaji mengi, wakiwa katika hali duni kabisa ya kimaisha, na watu waliotoroka makazi yao, ambapo mahitaji ya kijamii ni makubwa zaidi. Kwa hivyo mpango huu ambao tumezindua unakusudia kuwapatishia watu hawa vituo vya afya, shule na mambo mengine muhimu zaidi: visima vya maji, "amesema Mikailou Sidibé, mkuu wa idara ya miundombinu ya G5 Sahel.

Mwakilishi wa idara ya ushirikiano ya Ujerumani amethibitisha azma ya nchi yake ya kuimarisha msaada wake kwa amani katika ukanda wa Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.