Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

DRC: Dini zashindwa kuafikiana kuhusu nani atakeongoza CENI, licha ya muda kumalizika

Bado haijulikanii ni lini jina la mwenyekiti mpya wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini DRC, CENI, litajulikana. Muda wa mwisho wa masaa 72 uliotolewa na spika wa Bunge ulimalizika tangu Jumatatu, Oktoba 4.

Maafisa wa polisi wanasimama mbele ya jengo la Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi, CENI.
Maafisa wa polisi wanasimama mbele ya jengo la Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi, CENI. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Madhehebu ya kidini bado yamegawanyika juu ya kugombea kwenye nafasi hiyo kwa Denis Kadima, anayechukuliwa na baaadhi ya dini kuwa ana uhusiano wa karibu na rais wa jamhuri. Kanisa katoliki na Protestanti wanasema wako tayari kwa majadiliano, lakini madhehebu mengine sita yamebaini kuwa mazungumzo yamekwisha na amempendekeza Denis Kadima kuwania kwenye nafasi ya mwenyekiti wa CENI. Kutokana an utofauti hizo, mchakato huo umeingiliwa na mpasuko na matokeo yake yanonekana kuwa hayatokuwa na uhakika.

Mvutano ulianza kujitokeza baada ya Madhehebu sita kupendekeza jina la Denis Kadima , kuwa kiongozi mpya wa CENI.

Mwishoni mwa wiki iliyopita,  Baraza la kanisa Katoliki (CENCO) na lile la kiprotestani ECC yaliomba  madhehebu mengine 6 kuwasilisha jina jingine kwenye nafasi hiyo mbali na Denis Kadima.

Baada ya hatua hii ya viongozi hao wa dini kushindwa kuelewana, suala la kumpata kiongozi wa CENI sasa limerejea kwa uongozi wa bunge, na sasa viongozi hao wanataka wabunge kupitia ripoti zao na kuchukua hatua ambayo itamaliza mvutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.