Pata taarifa kuu
DRC-UCHUMI-NYUKI

Ufugaji na uvunaji wa asali kwa njia ya kisasa Wilayani Kabalo nchini DRC

Ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kupata asali, kwa ajili ya kiuchumi, umeanza kupata umaarufu katika eneo la Kabalo, mkoani Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ufugaji na uvunaji wa asali
Ufugaji na uvunaji wa asali NARINDER NANU AFP
Matangazo ya kibiashara

Kihistoria shughuli za ufugaji wa nyuki kwa ajili ya asali, imekuwa ikitekelezwa na makabila ya Twa na Bantu kwa ajili ya matumizi yao kama chakula kikuu na kuuza ili kujipatia kipato.

Hata hivyo,  wafungaji hao sasa wana cha kufurahia baada ya Shirika lisilo la kiserikali kutoka nchini Ufaransa, Apiflordev, kuwapa mbinu za kisasa za kufuga nyuki na kuvuna asali.

Medard Sibangolo, Mkuu wa kitengo cha Kilimo katika Wilaya ya Kabalo anaeleza kuhusu mbinu hii mpya.

Tunaangalia katika mziga huu wa  kuvuna asali, tunaufungua  na kupata asali ndani, sasa tunavuna.

Daniel Mbuyu, mmoja wa  mfugaji wa asali kutumia njia ya kisasa anaeleza manufaa ya njia hii mpya.

Njia za zamani zilikuwa zinachosha sana, kwa sababu ulitakiwa kwenda msituni na moshi na moto ili kupata nyuki, lakini kwa sasa tunaweza kufanya hili na kuwaacha nyuki na kuvua vizuri.

Londres Sango, afisa wa mipango kutoka  Shirika la Chakula na Kilimo FAO katika eneo hilo, anazungumzia manufaa ya mbinu hii ya kisasa.

Tunavuna asali mara mbili kwa mwaka. Tukipata kiwango kidogo hasa mwezi Aprili, tunapata Lita 15 kutoka kwenye kila mzinga. Lakini katika msimu mkubwa, tunapata Lita 15 hadi 20 na huo ni mwezi wa Oktoba.

Mpaka sasa, mizinga ya kuvuna  asali 570 imewekwa kwenye Wilaya ya Kabalo na sasa Shirika la FAO linasema, litafungua soko la asali  katika mji huo  ili kuimarisha biashara ya biadhaa hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.