Pata taarifa kuu
SENEGAL

Wahamiaji kadhaa waangamia katika pwani ya Senegal

Nchini Senegal, mtumbwi wa wahamiaji haramu karibu 60 ulizama ktika pwani ya Saint-Louis, kaskazini mwa nchi hiyo. Kwa sasa, Jeshi la Wanamaji limeweza kuokoa watu kumi na mmoja, wakiwemo Wasenegal wanane na raia watatu kutoka Gambia. Mwili wa mmoja wa wahamiaji hao pia umepatikana. Watu wengine hawajulikani walipo, kulingana na mmoja wa manusura.

Mitumbwi kwenye huko Soumbédioune, Dakar, Senegal, Novemba 2020.
Mitumbwi kwenye huko Soumbédioune, Dakar, Senegal, Novemba 2020. RFI/Charlotte Idrac
Matangazo ya kibiashara

Bilal ana umri wa miaka 24, yeye ni fundi cherehani huko Saint-Louis. Aliondoka Jumatano Agosti 25 kwa kutumia mtumbwi kuelekea Uhispania, bila hata hivyo kuifahamisha familia yake.

Lakini safari ilikatizwa asubuhi siku moja baadaye wakati mtumbwi ulianza kuingia maji kilomita 25 kutoka pwani ya Saint-Louis kwa sababu ulizidiwa uzito kutokana na wingi wa watu, amesema kijana huyo. “Maji mengi yaliingia katika mtumbwi. Nilichukua dumu la petroli na kuanza kuogelea. Na bahati nzuri nilipata msaada kutoka kwa mvuvi aliyenivuta kutoka kwa maji karibu saa 10 alfajiri. "

Visa vya uhamiaji haramu huanza kila mwaka wakati wa msimu wa joto licha ya vifo vingi ambavyo ni vigumu kuhesabu, amebaini Mame Latyr fall kutoka shirika la kiraia huko Saint-Louis.

Vikosi vya majinivinaendelea na shughuli za utaftaji na uokoaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.