Pata taarifa kuu
DRC

DRC: Serikali yapiga marufuku matumizi ya maji kutoka mito ya Kasai na Tshikapa

Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ujumbe wa kwanza wa serikali umezuru mkoa wa Kasai baada ya uchafuzi wa mito ya Kasai na Tshikapa na vitu vyenye sumu kutoka kampuni za madini kutoka Angola, ambapo kunapatikana vyanzo vya mito hiyo.

Mto Kasai.
Mto Kasai. DR
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano wa baraza la mawaziri siku ya Ijumaa, serikali iliwataka watu wasitumie maji machafu. Kwa sababu uharibifu ni mkubwa: maji yamepoteza rangi, viumbe vya majini vimekufa.

Eve Bazaba, Naibu Waziri Mkuu anayesimamia Mazingira, anaongoza ujumbe huu wa serikali katika mkoa huo. Kulingana na muhtasari wa mkutano wa Baraza la Mawaziri lililoongozwa na Waziri Mkuu Sama Lukonde, Naibu Waziri Mkuu anatarajiwa kujumuishwa katika saa zijazo na mawaziri wenzake wa Maendeleo Vijijini, Uvuvi, Maswala ya Jamii na pia afya ili kutoa msaada kwa raia, ambao ni waathiriwa wa uchafuzi huu.

Eve Bazaïba aliongoza jana mkutano wa baraza la usalama la mkoa na wawakilishi waliochaguliwa katika mkoa wa Kasaï. Eve Bazaïba amesema, hali hiyo imepitiwa "katika nyanja zote na mitazamo ya suluhisho la kudumu".

Haijulikani kwa muda gani raia hatatumia maji ya mito hiyo, wabunge katika mkoa wa Kasai wameelezea wasiwasi. Lakini Eve Bazaïba amehakikisha kuwa suluhisho za haraka zinazingatiwa kulinda raia.

Msaada wa matibabu kwa raia

Siku ya Ijumaa, mwenzake wa afya, Jean-Jacques Mbungani, aliliambia Baraza la Mawaziri juu ya usambazaji wa msaada wa vifaa, pamoja na vifaa vya matibabu vya dharura na vituo vya usambazaji wa maji kwa watu walioathirika.

Alibaini pia juu ya utambuzi endelevu wa maeneo yote ya afya yaliyo karibu na mito hiyo na familia zilizoathiriwa na uimarishaji wa ufuatiliaji wa magonjwa katika mkoa. Kwa sababu visa vya magonjwa yanayosababishwa na maji machafu vimeripotiwa.

Wakati huo huo, kulingana na Waziri Mkuu Jean-Michel Sama Lukonde, serikali imeitaka Angola kutathmini hali hiyo. Jambo kuu kwa Kinshasa ni kupata fidia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.