Pata taarifa kuu
DRC

Waziri wa zamani wa Afya Eteni Longondo awekwa kizuizini kabla ya kesi kuanza

Waziri wa zamani wa Afya wa DRC Eteni Longondo, aliyeshtakiwa kwa karibu mwaka mmoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (IGF) kwa kufuja pesa zilizotengwa kwa kudhibiti Covid-19 wakati alikuwa madarakani mwaka 2020, aliwekwa kizuizini Ijumaa, Agosti 27, 2021, katika jela la Makala, baada ya kusikilizwa katika ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu huko Kinshasa.

Waziri wa zamani wa Afya wa DRC Eteni Longondo, kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Kinshasa. Alikamatwa Ijumaa Agosti 27, 2021.
Waziri wa zamani wa Afya wa DRC Eteni Longondo, kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Kinshasa. Alikamatwa Ijumaa Agosti 27, 2021. © RFI / Pascal Mulegwa
Matangazo ya kibiashara

Ni kitendo kinachozidi kutoa sifa ya Rais Tshisekedi, amesema mmoja wa washauri wake wa karibu, ambaye alikasirika kuona mahakama inatuhumiwa kwa kuwafunga tu wapinzani wa serikali.

Eteni Longondo ni mtu muhimu katika chama cha rais, UDPS. Alikuwa alishafikishwa mahakamani na Mkaguzi Mkuu wa Fedha mwezi Agosti 2020, lakini kesi hiyo haikushughulikiwa, na hivyo kumuudhi mkuu wa IGF.

Mwanzoni mwa wiki hii, faili hiyo ilibadili mwelekeo. Eténi Longondo alifika katika ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu akiambatana na mawakili wake, Ijumaa, Agosti 27 mwendo wa saa 5 mchana .

 Chanzo kilicho karibu na ofisi ya mwendesha mashtaka kimebainisha kuwa alipelekwa gerezani kwa sababu kuna dalili kubwa za hatia zinazomkabili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.