Pata taarifa kuu
MALI-HAKI

Mali: Mawaziri wawili wa zamani wakamatwa kwa madai ya ufisadi

Waziri Mkuu wa zamani wa Mali Soumeylou Boubeye Maïga, pamoja na Waziri wa zamani wa Fedha na Uchumi wa nchi hiyo, wamefunguliwa mashitaka na kuwekwa chini ya hati ya kukamatwa na Mahakama Kuu, hasa katika kesi ya ununuzi wa ndege ya rais wa zamani Ibrahim Boubacar Keïta. Katika kesi hii, kama ilivyo kwa kesi zingine, watu kadhaa wanatarajiwa kukamatwa.

Soumeylou Boubeye Maïga, mnamo 2018 huko Bamako.
Soumeylou Boubeye Maïga, mnamo 2018 huko Bamako. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Soumeylou Boubeye Maïga alikuwa Waziri wa Ulinzi wa Mali wakati wa tukio hilo pamoja na Bi. Bouaré Fily Sissoko, Waziri wa Fedha na Uchumi.

Wawili hao walishtakiwa kwa ulaghai na kughushi hasa kuhusiana na kesi ya ununuzi wa ndege ya rais ambayo ilianza tangu miaka ya 2013-2014.

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Mali Soumeylou Boubeye Maiga tayari amekamatwa na anazuiliwa katika jela la kiraia la mjini Bamako na Bi. Bouaré Fily Sissoko, Waziri wa Fedha na Uchumi anazuiliwa katika jela la wanawake la Bollé huko Bamako.

Viongozi wa mashtaka wanasema wakati Maiga akiwa Waziri wa Ulinzi, aliongeza bei ya ununuzi wa ndege ya rais mwaka 2014, iliyonunuliwa kwa Dola Milioni 36.

Maiga mwenye umri wa miaka 67, alikuwa Waziri Mkuu wakati wa serikali ya Ibrahim Boubacar Keita, iliyoondolewa madarakani na Kanali Assimi Goita mwezi Agosti mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.