Pata taarifa kuu
DRC

DRC: Mwanasiasa Gabriel Kyungu Wa Kumwanza aaga dunia

Gabriel Kyungu Wa Kumwanza, mmoja kati ya waanzilishi wakuu wa chama cha UDPS mwanzoni mwa miaka ya 1980 na mshirika wa karibu wa Félix Tshisekedi, rais wa sasa wa DRC, alifariki dunia Jumamosi hii, Agosti 21 huko Luanda, nchini Angola.

Gabriel Kyungu Wa Kumwanza alifariki Jumamosi hii, Agosti 21, 2021 huko Luanda.
Gabriel Kyungu Wa Kumwanza alifariki Jumamosi hii, Agosti 21, 2021 huko Luanda. AFP - JUNIOR KANNAH
Matangazo ya kibiashara

Gabriel Kyungu alikuwa kiongozi asiyekuwa na msimamo kamili, ambaye aliweza kubadili vyama kutokana na hali ya kisiasa ilivyo ikijiri nchini DRC.

Gabriel Kyungu alijiunga na siasa tangu miaka ya 1960. Gabriel Kyungu ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha wafanyakazi katika elimu, alijikuta akishirikiana na Étienne Tshisekedi Wa Mulumba kati ya waanzilishi wakuu kumi na tatu wa chama cha UDPS, wabunge ambao walijitenga na Mobutu mwanzoni mwa miaka ya 1980. Baadaye, alibadili msimamo na kujiunga na Marshal Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga.

Gabriel Kyungu Wa Kumwanza ni mmoja wa wachochezi wakuu wa mauaji ya kikabila ambayo yalilenga watu kutoka Kasai, ambao walilazimika kuondoka Katanga miaka ya 1990. Baada ya kundi la waasi la AFDL, la Laurent-Désiré Kabila kuchukuwa madaraka, aliungana na utawala mpya kabla ya kurrejea katika kambi ya upinzani.

Aliungana tena na Étienne Tshisekedi kabla ya kifo cha baba wa rais wa sasa wa DRC, Felix Tshisekedi. Hadi kifo chake akiwa na umri wa miaka 83, alikuwa mmoja wa washirika wakuu wa Felix Tshisekedi.

Gavana wa zamani wa Katanga Moïse Katumbi anapongeza kazi ya mwanasiasa huyo ambaye aliwahi kuwa spika wa Bunge la Jimbo la Katanga wakati wa uongozi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.