Pata taarifa kuu
DRC-HAKI

DRC: Wafungwa 150 wafariki dunia ndani ya kipindi cha miezi 6

Shirika linalotetea haki kwa wote nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Acaj, linalalamikia dhidi ya mazingira wanakozuiliwa wafungwa.

Gereza la Makala, nchini DRC.
Gereza la Makala, nchini DRC. AFP PHOTO / JUNIOR D. KANNAH
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake ya hivi karibuni, Acaj linasema limeamua kupaza sauti ili kuona kuwa serikali inawezakufanya chochote kukabiliana na hali hiyo, inayosababisha madhara makubwa kwa wafungwa, licha ya maboresho kadhaa.

Ukosefu wa huduma inayofaa ya matibabu, msongamano na hali ya kimazingira kwa wafungwa wanaozuiliwa: hizi ni sababu ambazo Acaj inaelezea kuwa zinasababisha vifo katika gereza la Makala jijini Kinshasa tangu mwanzoni mwa mwakahuu. Gereza lililojengwa tangu enzi za ukoloni, ambalo lina uwezo wa kupokea wafungwa 1,500, lakini mwishoni mwa mwezi Julai 2021, lilikuwa na zaidi ya wafungwa 9,000. Zahanati katika jela hilo haina vifaa vya kutunza wafungwa wagonjwa, vile vile kituo cha matibabu cha Sanatorium ambacho wafungwa hawa huhamishwa kila mara wanapozidiwa na magonjwa.

Acaj imeelezea wasiwasi wake kutokana na mazingira wanakozuiliwa wanawake. Kwa sasa wanawake 186 ndio wanazuiliwa katika jela la Makala. Wanne kati yao wana watoto wachanga. Acaj imeitaka serikali kupunguza msongamano wa wafungwa, kwa kujenga jela mpya za kisasa zinazoendana na viwango vya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.