Viongozi wa Afrika wamuenzi Kenneth Kaunda
Mazishi ya kitaifa kumwaga aliyekuwa rais wa kwanza na mwanzilishi wa taifa la Zambia, Kenneth Kaunda, aliyefariki dunia mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 97, yamefanyika leo jijini Lusaka.
Imechapishwa:
Maelfu ya waoombolezaji waliwasili katika uwanja wa Mashujaa kumwaga Kaunda, kiongozi huyo wa zamani ambaye ndiye aliyekuwa anasalia kama mmoja wa vigogo waliopigania uhuru barani Afrika.
Mwili wa Kaunda, ulibebwa na wanajeshi wa taifa hilo huku Jenereza lake likifunikwa na bendera ya nchi hiyo na kupewa heshima kwa kupigwa mizinga 21.
Viongozi mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika wamehudhuria mazishi haya, na kumsifu Kaunda katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa mataifa ya Afrika hasa yale yaliyo eneo la Kusini yanakuwa huru.
Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Africa mashariki, akisemtaja kaunda Kaunda kama kiongozi aliyesimamia haki.
Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mouusa Faki kwa upande wake alimkumbuka Kaunda kama, nguzo muhimu aliyeanzisha Umoja umoja wa Africa.
Kaunda, ambaye alifahamika kama KK alitawala nchi hiyo kwa miaka 27 tangu Uhuru wa nchi hiyo mwaka 1964 na atazikwa tarehe 7 mwezi Julai.