Pata taarifa kuu
MALI - USALAMA

Mali - UN yaongeza muda wa wanajeshi wake kuhudumu

Baraza la usalama la umoja wa mataifa, limeongeza muda wa wanajeshi wake kuhudumu nchini Mali, hadi Juni mwaka ujao wa 2022.

Rais wa serikali ya mpito ya Mali, Col. Assimi Goita
Rais wa serikali ya mpito ya Mali, Col. Assimi Goita AP
Matangazo ya kibiashara

Baraza hilo limesisitiza haja ya serikali kurejeshwa kwa raia kupitia uchaguzi ambao umeratibiwa Feb 27 mwakani.

Hatua hii ya hivi punde ya umoja wa mataifa unakuja baada ya Ufaransa kutangaza kusitisha usaidizi wa kijeshi kwa nchi ya Mali kupitia ujumbe wa Barkhane.

Azimio hilo pia limemtaka katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Antonio Guterres, kuwasilisha ripoti kabla ya tarehe 15 julai kuhusu hali ya utovu wa usalama na vurugu dhidi ya raia nchini mali.

Umoja huo aidha umeitaka serikali ya mpito ya Mali kuandaa uchaguzi wa huru na haki pamoja na kura ya maoni kuhusu katiba mnamo Febuari mwaka ujao

Mbali na hayo, umoja huo umesisitiza kwamba rais wa sasa wa mpito, naibu wake pamoja na waziri mkuu wa mpito, kwa vyovyote vile hawapaswi kuwa wagombea katika uchaguzi mkuu ujao.

Nchi ya Mali imeendelea kushuhudia utovu wa usalama kutoka kwa makundi ya kijihadi, licha ya uwepo wa majeshi ya Ufaransa na Umoja wa mataifa, hali ambayo kwa sasa imeenea katika mataifa ya Burkina Faso na Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.