Pata taarifa kuu
UGANDA-CORONA

Uganda imeidhinisha matumizi ya Covidex dawa ya kienyeji

Uganda imeidhinisha matumizi ya Covidex dawa ya kienyeji, kusaidia kutoa tiba kwa watu walioambukizwa virusi vya Covid 19 nchini humo.

Muuguzi nchini Uganda akijianda kutoa chanjo
katika hospitali ya Mulago huko Kampala, Machi 10, 2021
Muuguzi nchini Uganda akijianda kutoa chanjo katika hospitali ya Mulago huko Kampala, Machi 10, 2021 AFP - BADRU KATUMBA
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya kuidhiniza dawa nchini humo David Nahamya, amesema dawa hiyo sio tiba, bali inatumiwa na dawa nyingine zinazopewa wagonjwa wa virusi hivyo.

00:28

OUGANDA _Son Uganda: Approves use of herbal medicine to treat viral infections-Sound, David Nahamya National Drug Authority

Mpaka sasa, hakuna dawa au tiba iliyopatikana kutibu maambukizi ya Corona na baadhi ya tiba za kiasili ambazo zimekuwa zikipatikana barani Afrika, hazijaidhinishwa Kisayansi na Shirika la afya duniani WHO.

Uganda kwa sasa inakabiliwa na wimbi la pili la maambukizi ya Covid 19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.