Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

CAR yaomba msamaha Chad baada ya shambulio kwenye mpaka

Siku mbili baada ya ya kituo cha maafisa wa Chad mpakani kushambuliwa na jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui imekiri kosa na kuomba msamaha . Ujumbe ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya nje Sylvie Baïpo Temon ulipokelewa Jumanne Ndjamena na rais wa Baraza la Jeshi la Mpito na nchi hizo mbili ili kubaini mazingira ya shambulio hili.

Jamhuri ya Afrika ya Kati imelaani "vikali" shambulio la jeshi lake kwenye kituo cha maafisa wa Chad cha mpakani , shambulio lililosababisha vifovya askari sita wa Chad Jumapili (picha ya kumbukumbu)
Jamhuri ya Afrika ya Kati imelaani "vikali" shambulio la jeshi lake kwenye kituo cha maafisa wa Chad cha mpakani , shambulio lililosababisha vifovya askari sita wa Chad Jumapili (picha ya kumbukumbu) © AFP/FLORENT VERGNES
Matangazo ya kibiashara

Jamhuri ya Afrika ya Kati imelaani "vikali" shambulio la jeshi lake kwenye kituo cha mpakani nchini Chad, shambulio ambalo lilisababisha vifo vya wanajeshi sita wa Chad siku ya Jumapili, ikiwa ni pamoja na watano "waliotekwa nyara na kuuawa", wakati wa mkutano Jumanne jioni huko Ndjamena kati ya mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi hizi mbili. Pande hizi mbili "ziliafikiana kubaini mazingira ambamo shambulio hili lilitekelezwa", kulingana na taarifa ya pamoja.

Ujumbe wa Afrika ya Kati ulipokelewa na rais wa Baraza la Jeshi la Mpito mara tu baada ya kuwasili kwake, na kumfikishia ujumbe rais Mahamat Idriss Deby Itno.

Nchi hizo mbili "zilikubaliana kuanzishwa kwa tume huru ya kimataifa ya uchunguzi na isiyo na upendeleo " itakayoundwa na Umoja wa Mataifa na mashirika ya kikanda ambayo yafika eneo la shambulizi na kutoa ripoti ambayo itabaini wahusika na wajibu wa kila mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.